Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria
uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa itakayotumia
umeme Standard Gauge (SGR) itakayotoka mkoani Morogoro hadi Makutupora
Dodoma katika eneo la Stesheni ya Ihumwa nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Wengine katika picha ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na Balozi wa
Uingereza hapa nchini Sarah Cooke wakishuhudia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunua kitambaa wakati
akiweka jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa itakayotumia
umeme Standard Gauge (SGR) itakayotoka mkoani Morogoro hadi Makutupora
Dodoma katika eneo la Stesheni ya Ihumwa nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunga kifuniko mara
baada ya kutumbukiza karatasi ya majina ya viongozi mbalimbali
waliofanikisha ujenzi huo kama kumbukumbu katika uwekaji wa jiwe la
msingi la Reli ya Kisasa(SGR) itakayotoka mkoani Morogoro-hadi
Makutupora Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saruji
iliyochanganywa na kokoto kwenye jiwe hilo la msingi la ujenzi wa Reli
ya Kisasa kutoka mkoani Morogoro-hadi Makutupora Dodoma yenye urefu wa
km 422 katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saruji
iliyochanganywa na kokoto kwenye jiwe hilo la msingi la ujenzi wa Reli
ya Kisasa kutoka mkoani Morogoro-hadi Makutupora Dodoma yenye urefu wa
km 422 katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
akiweka saruji iliyochanganywa na kokoto kwenye jiwe hilo la msingi la
ujenzi wa Reli ya Kisasa mkoani Morogoro-hadi Makutupora Dodoma yenye
urefu wa km 422 katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa ya
umeme kutoka mkoani Morogoro-hadi Makutupora Dodoma yenye urefu wa km
422 katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma. Wengine katika picha
ni Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano Pro. Makame Mbarawa, Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Reli
TRC Masanja Kadogosa pamoja na viongozi wengine.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua mfano wa Reli hiyo
ya Kisasa itakayotumia umeme mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika
eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua mfano wa Reli hiyo
ya Kisasa itakayotumia umeme mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika
eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya
wabunge waliofika kwenye uzinduzi wa Reli hiyo ya Kisasa SGR itakayo
toka Morogoro hadi Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi mara
baada ya kuweka jiwe la msingi la Reli hio ya Kisasa katika eneo la
Ihumwa Stesheni mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwashukuru madereva wa
magari yatakayofanya kazi ya ujenzi wa reli hiyo ya kisasa SGR itakayo
toka Morogoro hadi Dodoma.
Sehemu ya wananchi mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo za uwekaji wa jiwe la msingi.
Treni ya zamani ikipita katika Reli za zamani katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi
wakati akiwasili katika eneo la Ihumwa Stesheni kwa ajili ya uwekaji wa
jiwe la msingi.
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Reli
TRC Masanja Kadogosa akitoa maelezo ya mradi huo wa Reli ya kisasa ya
umeme kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli PICHA NA IKULU