SERIKALI YAJIPANGA KUWAJENGEA UWEZO WATOA HUDUMA KATIKA SEKTA YA UTALII NA UKARIMU NCHINI

February 16, 2018


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki akizungumza na  wadau wa sekta ya  utalii waliokutana jana katika mkutano uliofanyika jana mjini Dodoma   kwa ajili ya kupitia Rasimu ya kanuni za kusimamia ubora wa huduma katika sekta ya ukarimu na utalii


 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Deograsias Mdamu ( wa kwanza kulia) akimkaribisha  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki (katikati) kwa ajili ya  kuzungumza na  wadau wa sekta ya  utalii waliokutana jana katika mkutano uliofanyika mjini Dodoma   kwa ajili ya kupitia Rasimu ya kanuni za kusimamia ubora wa huduma katika sekta ya ukarimu na utalii


Baadhi ya wadau wa sekta ya utalii  wakifuatilia  uwasilishaji wa Rasimu ya kanuni za kusimamia ubora wa huduma katika sekta ya ukarimu na utalii katika mkutano uliofanyika jana mjini Dodoma   uliowakutanisha wadau wa sekta hiyo kwa ajili ya kupitia rasimu hiyo.



Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utalii, Paskas Mwiru  akizungumza na  wadau wa sekta ya  utalii waliokutana jana katika mkutano uliofanyika mjini Dodoma   kwa ajili ya kupitia Rasimu ya kanuni za kusimamia ubora wa huduma katika sekta ya ukarimu na utalii



Baadhi ya  wakurugenzi wasaidizi  wakifuatilia  uwasilishaji wa Rasimu ya kanuni za kusimamia ubora wa huduma katika sekta ya ukarimu na utalii katika mkutano uliofanyika jana mjini Dodoma   uliowakutanisha wadau wa sekta ya Utalii kwa ajili ya kupitia rasimu hiyo.



Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Deograsias Mdamu akisisitiza jambo  katika mkutano uliofanyika jana mjini Dodoma kati ya Wadau wa sekta ya utalii na Wizara  kwa ajili ya kupitia Rasimu ya kanuni za kusimamia ubora wa huduma katika sekta ya ukarimu na utalii



Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Viwoso  Mkwizu akiwasilisha Rasimu ya kanuni za kusimamia ubora wa huduma katika sekta ya ukarimu na utalii katika mkutano uliofanyika jana mjini Dodoma   uliowakutanisha wadau wa sekta ya Utalii kwa ajili ya kupitia rasimu hiyo. ( PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-MNRT)

Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imewasilisha  rasimu ya   kanuni ya kusimamia watoa huduma katika sekta ya utalii na ukarimu kwa wadau wa sekta hiyo  ili waweze kutoa maoni yao  yatakayosaidia katika kuboresha kanuni hizo ili ziweze kuwasimamia wafanyakazi  kwa kuhakikisha kuwa  huduma zinazotolewa   zinazokidhi viwango vya kimataifa kwa watalii.

Akizungumza  jana mjini Dodoma kwenye  mkutano uliowakutanisha wadau wa sekta hiyo  kwa ajili ya kupitia Rasimu ya kanuni hiyo,  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki alisema Wizara imeandaa rasimu hiyo  ili kutoa nafasi kwa wadau  kuipitia na kutoa maoni yatakayoisaidia katika kuiboresha.

Akizungumzia moja ya  lengo la kanuni hizo ni  kutaka  kuwajengea uwezo wafanyakazi wa tasnia hiyo ili waweza kushindana katika soko la ajira la kitaifa na kimataifa.

Aliongeza kuwa kanuni hizo  pia  zitasaidia  kuwawekea ulinzi na usalama katika taaluma hiyo pamoja na kuleta uwajibikaji na uaminifu katika kutoa huduma kwa vile kutakuwa na  mfumo wa kuwatambua.

Alisema hatua hiyo ya ukusanyaji maoni  imekuja baada ya sekta hiyo ya  kukabiliwa na changamoto ya huduma hafifu zinazotolewa kwa watalii hususani wale wa kimataifa.

Alisema hali hiyo imechangiwa na ukosefu wa chombo cha kusimamia viwango vya huduma zinazotolewa katika sekta hiyo.

Alisema kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu kutoka watalii kuwa huduma wanazopata ni hafifu.

Awali, Mkurugenzi wa idara ya Utalii, Deograsias Mdamu, alisema majadiliano hayo  ya kuboresha  kanuni hizo yatasaidia kuwa na wafanyakazi mahiri na wenye weledi katika tasnia hiyo.

Aliongeza kuwa,  maoni hayo yatapelekea kuunda kanuni bora na shirikishi zitakazosaidia  katika kuwasimamia wafanyakazi na waajiri  katika kutoa huduma  bora kwa watalii kwa kila mmoja kwa nafasi yake.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama cha waongoza watalii Tanzania, Emannuel Mollell aliipongeza Wizara kwa hatua h iliyofikia ya kuandaa rasimu hiyo kwa vile rasimu hiyo  inatoa muelekeo mzuri  katika sekta ya utalii na ukarimu nchini.

Akichangia maoni Katibu huyo , Emanuel Molleli alisema ni vyema  kanuni  igusie maslahi ya wafanyakazi    kwani hicho kimekuwa  ni kilio chao cha  muda mrefu lakini katika  rasimu hiyo hakuna kipengele chochote kilichozungmzia suala hilo.

Aliongeza kuwa  wafanyakazi wa tasnia hiyo kwa ujumla wake  wamekuwa wakilipwa mshahara midogo sana hali inayoplekea kushusha morali katika kuwahudumia watalii kwa viwango bora.

 Kutokana na uwasilishwaji wa maoni hayo , hali hiyo ilimfanya   Mkurugenzi wa Idara ya hiyo, Mdamu kumjibu    kuwa suala hilo litaangaliwa.

Naye, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Bety Begashe wakati akichangia maoni aliiomba  Wizara iiangalie namna bora itakayosaidia kutoa mafunzo kwa wafanyakazi hao mbali na mitihani itakayokuwa inafanywa na wanatasnia hao.
 

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »