WANANCHI WAHIMIZWA KUTUMIA LANDMAX KUEPUKA UTAPELI WA ARDHI

June 24, 2026

Na Hamida Ramadhan,Dodoma

MBUNGE wa Jimbo la Mbozi, Onesmo Mnkondya, amewataka wananchi na madalali wanaohusika na biashara ya ardhi kutumia huduma za Landmax Real Estate Company Limited ili kufanya uwekezaji kwa usalama na kuondokana na migogoro inayotokana na mauzo au ununuzi usio rasmi wa ardhi.

Mnkondya, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Landmax Real Estate Company Limited, amesema hayo Juni 24, 2026 jijini Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofisi za kampuni hiyo.

Amesema Landmax imeanzishwa kwa lengo la kuwasaidia wananchi kupata ardhi salama na makazi bora huku ikichangia kupunguza migogoro ya ardhi.

Aidha, amebainisha kuwa kampuni hiyo inatoa huduma mbalimbali ikiwemo uuzaji na ununuzi wa ardhi na mali isiyohamishika, ushauri wa uwekezaji wa ardhi, usimamizi wa mali, urasimishaji wa nyaraka za ardhi, uendelezaji wa miradi, tafiti za soko pamoja na ushirikiano katika miradi ya maendeleo.

“Tunawaalika wananchi na madalali wote wanaotaka kununua au kuuza ardhi kufika ofisini kwetu ili wapate huduma bora na salama,” amesema Mnkondya.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, amezitaka Halmashauri zote za Mkoa huo kufanya kazi kwa kasi na ufanisi ili kuendana na kasi ya wawekezaji wa sekta binafsi.

Amesema ucheleweshaji wa huduma kwa wawekezaji unaweza kudhoofisha maendeleo ya uchumi wa Taifa na kuathiri mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya nchi.

“Ukiichelewesha sekta binafsi, unakuwa unadhoofisha mchango wao katika ujenzi wa Taifa ni muhimu Halmashauri na taasisi nyingine za umma kufanya kazi kwa kasi inayolingana na wawekezaji,” amesema Senyamule.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, Clayton Chipando, amewataka wananchi kutumia huduma za Landmax Real Estate Company Limited ili kujiepusha na matapeli wanaojihusisha na biashara za ardhi na mali isiyohamishika.

Amesema matukio ya utapeli yamekuwa yakiongezeka kutokana na baadhi ya watu kutumia njia zisizo rasmi katika miamala ya ardhi, hivyo ni muhimu wananchi kutumia kampuni zinazotoa huduma za kitaalamu na zinazofuata taratibu za kisheria.

“Ndugu zangu kama mnavyojua matapeli siku hizi wamekuwa wengi na wajanja, hivyo ili kuwa salama tumieni kampuni ya Landmax,” amesema Baba Levo

Ameongeza kuwa" Kupitia huduma za kitaalamu zinazotolewa na kampuni hiyo, wananchi watapata uhakika wa umiliki wa ardhi na kufanya uwekezaji wao kwa kujiamini zaidi, " Amesema.








 

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »