AFRICAN SPORTS KUWEKA KAMBI VISIWANI ZANZIBAR

February 13, 2018
TIMU ya African Sports "Wanakimanumanu"inatarajiwa kuelekea Visiwani Zanzibar kuweka kambi kwa ajili ya kujiwinda na michuano ya Ligi Daraja la pili msimu ujao.
Akizungumza juzi,Mwenyekiti wa timu hiyo,Awadhi Pamba alisema watakwenda hukobaada ya kufanya mawasiliano na ukoo wa familia ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar Abeid Karume.

Alisema sababu za kuweka kambi visiwani humo ni kumuenzi Mzee Karume kwa sababu naye alikuwa na timu yake inaitwa African Spots na walikuwawakienda kucheza nao kila wakati hivyo wanataka kurudisha enzi hizo.

"Ukiangalia sisi zamani tulikuwa tunatembeleana African Sports ya Tanga na ile ya  Zanzibar kwani undugu wetuni wa damu ambao ni wa siku nyingi lakini hata Klabu ya Yanga undugu wetu umeimarika mwaka jana tukiwa daraja la kwanza walikwenda kupiga kambi klabu ya Yanga "Alisema

Akizungumzia mikakati ya usajili,Mwenyekiti huyo alisema mipango yao mikubwa ni kuhakikisha wanachukua wachezaji wenye uwezo wanaoweza kucheza ligi daraja la pili na kwanza kwa lengo la kukiimarisha kikosi chetu"Alisema.

Hata hivyo alisema kabla ya kuanza usajili wataunda kamati ya usajili ambayo itakuwa na jukumu la kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwawaledi mkubwa.

Mwenyekiti huyo alisema wanamshukuru Waziri wa Afya,Maendeleo yaJamii,Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu kwa kushirikiana na wafadhili wengine wakiwemo GBP na Mwafrika Phamary kuisaidia timu hiyo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »