KAMATI YA USAJILI COASTAL UNION KUTUA KENYA

February 13, 2018
KAMATI ya Usajili ya Klabu ya Coastal Union imepanga kubisha hodi  nchini Kenya na Visiwani Zanzibar kuweka kambi kwa ajili ya kusaka baadhi ya wachezaji watakaokitumikia kikosi hicho msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

Akizungumza na Tanga Raha Blog,Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili,Hemed Aurora (Aliyekaa kulia) alisema kamati hiyo inatarajiwa kukutana baada ya kumalizika sherehe za kuwapongeza wachezaji wa timu hiyo kwa kuipandisha timu hiyo.

Alisema baada ya kumalizika kwa sherehe hizo Kocha Mkuu wa timu hiyo,Juma Mgunda atawakabidhi ripoti itakayokuwa na mahitaji kwa ajili ya kikosi hicho na nafasi zinazohitajika.

“Kama unavyojua timu yetu imepanda daraja hivyo tunahitaji kuanza maandalizi mapema ikiwamo suala la usajili na hapa inabidi tuwe makini maana tukikosea tutashindwa kufanya vizuri hivyo tutakwenda Zanzibar kusaka baadhi ya wachezaji “Alisema Aurora.

Hata hivyo alisema kamati hiyo imejipanga vilivyo kuhakikisha wanasaka wachezaji watakaoweza kuipa mafanikio timu hiyo ikiwemo kuipa ubingwa msimu ujao.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »