Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizingumza na wananchi wa
kijiji cha Kiziko alipofanya ziara katika jimbo la Mkuranga.
Mwenyekiti
wa Halmshauri ya Mkuranga, Juma Abeid akizungumza na wananchi wa kijiji
cha Kiziko juu ya mikakati ya Halmashauri katika uboreshaji wa sekta
mbalimbali.
Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwasili katika kijiji cha
cha Kitonga katika ziara ya vijiji jimbo la Mkuranga.
Na Chalila Kibuda,Globu ya jamii.
NAIBU
waziri wa Mifugo na Uvuvi (Mbunge) wa Jimbo la Mkuranga mkoani Pwani
Abdalla Ulega ametoa agizo kwa Watendaji wa vijiji na Wenyeviti
kuwasomea mapato na matumizi wananchi wao ili kuepuka kurudisha nyumba
uchangiaji wa shughili za maendeleo.
Naibu
waziri huyo ametoa agizo hilo wilayani humo akiwa katika mwendelezo wa
ziara za vijijini ambapo akiwa katika kijiji cha Kiziko, kilichopo Kata
ya Mwarusembe baada ya kupokea malalamiko ya wananchi juu ya viongozi
wao ngazi ya kijiji kushindwa kusoma taarifa ya mapato na matumizi.
Alisema
kushindwa kusoma taarifa za mapato na matumizi kunachangia kwa asilimia
kubwa wananchi kushindwa kuchangia maendeleo katika maeneo hayo hivyo
lazima wananchi wajulishe kinachoingia na kinavyotumika.
"Natoa
agizo hili kwa watendaji na wenyeviti kusoma mapato na mapato na
matumizi na hapa naagizi mtendaji wa Kata ya Mwarusembe kuhakikisha hadi
kufika Januari 2 ,2018 niwe nimepata taarifa za kushindwa kusoma mapato
na matumizi katika kijiji hiki cha kiziko. "alisema Ulega
Alisema
wananchi wanatamani kujitolea kwa lengo la kuchangia maendeleo lakni
wanavunjwa moyo viongozi hao huku akisisitiza kupewa ifika January 2 awe
amepata taarifa nakuhaidi kulifuatilia jambo hilo kwa ukaribu zaidi.
Pia
akiwa katika kijiji hicho cha alitoa mifuko 50 ya saruji pamoja na
shilingi laki tano kwa ajili kuchangia ujenzi ya serikali ya kijiji
hicho ikiwa pamoja na matundu ya vyoo katika shule ya msingi kiziko huku
akitoa ahadi ya shilingi tisa. Kwa ajili ya kuchangia vikundi tisa vya
Vikoba.
Awali
wakitoa kero zao kwa Mbunge huyo walisama wamakerwa sana na kukithiri
kwa mifugo aina ya ng'ombe hali inayosababisha umasikini na njaa kwa
wananchi hao kutokana na mazao yao.Pia
walilalamikia kukosekana kwa barabara, inayounganisha kijiji hicho cha
kiziko na vijiji vingine pamoja na Daraja linalounganisha vitongoji vya
Gwanzo, Chakande vyenye wakazi wengi zaidi.
"kwakweli
tuna kero nyingi mno hapa kijijini kwetu kwani mbali na barabara na
Daraja lakini pia tunakero ya kukosa Daktari kwenye Zahanati hii yetu
hali inayosababisha wananchi kukosa kupatiwa huduma stahiki.
"alisisitiza Mojamed Ally mjumbe wa serikali ya kijiji.
Naye
Ofisa Kilimo wa Kijiji hicho... Alisema wananchi hao ambao waliowengi ni
wakulima lakini wanakosa dhana za kisasa za kilimo pamoja na ukosefu wa
gereta ili kusikuma maji kwenye kisima cha maji kilichopo shule ya
msingi kiziko ili wanafunzi na raia wengine wapate maji.
Mbali
na kijiji hicho pia Naibu waziri Ulega aliendelea na ziara katika kijiji
cha Kitonga kata hiyo ya Mwarusembe ambapo pia alipokea kero ya
kuvamiwa na ng'ombe kwenye mashamba ya wananchi huku wakimtaka kumaliza
kero hiyo.
Wakati
huohuo wananchi hao walilalamika kwa Kiongozi wao huyo juu ya
kutoridhishwa na huduma zinazotolewa katika Hospitali ya wilaya hiyo
nakudai kwamba wakinana mama wanapohitaji kujifungua kuambiwa wabebe
vifaa vya uzazi mbali Serikali kusema huduma hiyo bure.
"Naibu
waziri kwakweli wananchi wako sisi tunaumia. Pale Hospitali ya Wilaya
ya mkuranga ni tatizo bado panafigisu na kona kona nyingi tunaomba
tusaidie. "alisema mmoja wa wananchi katika mkutano huo.