VIONGOZI WA KIJIJI CHA MSOSA WILAYANI KILOLO WAVULIWA MADARAKA KWA NGUVU

December 19, 2017
Mtendaji wa kata ya Ruaha Mbuyuni Maiko Chabili akiwafafanulia jambo wananchi wa kijiji wakati wa mkutano wa hadhara ulikuwa na lengo la kuwafukuza kamati ya mipango na fedha ya kijiji kwa matumizi mabaya ya pesa zao
 Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha msosa kilichopo tarafa ya ruaha mbuyuni walihudhuria mkutano wa hadhara wa kijiji

Na Fredy Mgunda,Iringa.


Wananchi wa kijiji cha msosa kilichopo tarafa ya ruaha mbuyuni wameifukuza kamati ya mipango na fedha kwa tuhuma za kufanya ubadhilifu wa mali za kijiji na kuunda kamati mpya itakayoleta maendeleo katika kijiji hicho.

Wakizungumza wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho wanachi waliutaka uongozi wa kamati hiyo kuachia ngazi kutokana na tuhuma zinazowakabili.

 Kwa upande wake mtendaji wa kata MAIKO CHABILI ameafiki kuvuliwa madaraka kwa viongozi wa kamati ya mipangano na fedha kutokana na tuhuma zinazowakabili.

Hata hivyo kamati ya mipango na fedha ya kijiji cha msosa walikubali kujiudhuru na kulipa pesa ambazo ilibaini kuwa walizitumia vibaya bila ruhusa ya wananchi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »