NAIBU WAZIRI MHE.MANYANYA AFUNGUA RASMI MKUTANO WA VIDEO CONFERENCE

December 18, 2017

DSC_0011
Naibu Waziri Mhe. Injinia Stella Manyanya afungua rasmi mkutano kwa njia ya Mtandao yaan (Video Conference) wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Mamlaka za mikoa na Halmashsauri za Wilaya kuhusu masuala ya sekta ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja na taasisi zake leo Tarehe 18 – 20 Disemba, 2017 na kuunganisha wadau kutoka mikoa ya Mbeya, Songwe, Kilimanjaro, Ruvuma, Kigoma, Lindi, Singida, Pwani na Dodoma.
Mhe. Naibu Waziri aliwashukuru Makatibu Tawala wa Mikoa, Wasaidizi wao na Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya ambao wameitikia wito pamoja na wataalamu na maafisa mbalimbali.
Wizara ilianza na taasisi yake ya BRELA ambayo ilielezea majukujumu yake na huduma mbalimbali wanazotoa kwa umma na kutoa fursa ya wadau kutoka mikoa yote iliyoshiriki walipata fursa ya kuuliza maswali na kujibiwa papo kwa papo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »