Na Mahmoud Ahmad Arusha
Naibu waziri wa mawasiliano na
uchukuzi Afashasta Nditie amezindua Mkutano mkuu wa kujadili mfumo wa
Anuani za makazi uliofanyika mkoani Arusha ambao umewakutanisha wadau
mbali mbali wa mawasiliano kutoka barani Africa .
Akizungumza na wadu hao Naibu
waziri Nditie amesema kuwa mfumo huo kwa hapa nchini upo vizuri na
anaamini kuwa mamlaka husika ipo makini katika kukamilisha hatua
iliyobaki ambayo itaifanya Tanzania kufika mbali.
Aliongeza kuwa mbali na jitihada
mbalimbali zinazofanyika kuweza kufikia kila moja lakini bado kuna
changamoto mablimbali za kuwepo na mitaa mingi isiyokuwa na majina ili
kuweza kurahisisha huduma ya posta mlangonii.
Kwa upande wake Kaimu
Posta mkuu wa shirika la Posta Tanzania Hassani Mwang’ombe
amesema kuwa hivi sasa wako katika mpango wa huduma ya posta mlangoni
ili kuweza kurahisisha barua zote kumfikia kila mmoja mwananchi mahali
anakoishi ili kuweza kupata mawasiliano.
Hata hivyo amesema kuwa
watanzania watajiskia vizuri na kuona furaha pindi watakapo ona huduma
ya posta inawafikia mpaka milangoni mwao kwani siwananchi wote wanaweza
kumudu kwenda mahli paliko huduma ya posta ili kuweza kuwasaidia maelfu
ya wakazi walio wengi.
Kwa upande wake katibu mkuu wa
Papu Younoss Djibrine alisema kuwa nimwanzo mzuri wa na njia nzuri kwa
nchi ya Tanzania kuweza kuanza huduma hii ya anuani na majina ya mtaa
ambapo hata united nation nihaki ya kila mmoja kuweza kupata utambuzi
wanakoishi lli kuweza kuwafuikia kirahisi zaidi.
Aliongeza kuwa nchi nyingi za
afrika zinachangamoto mbalimbali kiwemo kukosa anuiani za makazi yao
hali ambayo kuwafikia inakuwa vigumu sana lakini kuna haja za makusudi
kuweza nchi husika kuweza kuanzisha utaratibu huo.