Naibu Waziri wa Wizara mpya ya
nishati Subira Mgalu akizungumza na watendaji wa shirika la umeme
Tanesco Mkoa wa Pwani pamoja na wakandarasi baada ya kukagua mradi wa
REA awamu ya tatu uliopo maeneo ya sofu mlandizi Wilayani Kibaha
mkoani Pwani alipofanya ziara yake ya kikazi ya siku moja kwa ajili ya
kujionea mwenendo mzima wa ujenzi.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Naibu Waziri wa nishati Subira
Mgalu wa kati kati akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Tanesco Mkoa wa
Pwani Martin Madulu wa kushoto katika alipotembelea kituo cha usambazaji
wa umeme kilichopo Mlandizi.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Naibu Waziri wa Wizara mpya ya
nishati Subira Mgalu akipata ufafanuzi kutoka kwa wakandarasi wa mradi
wa umeme wa REA awamu ya tatu katika eneo la Msufini Mlandizi Wilayani
Kibaha Mkoa wa Pwani.
Naibu waziri mpya wa Nishati
Subira Mgalu akisikiliza kwa umakini maelezo kutoka kwa Meneja wa
tanesco Mkoa wa Pwani Martin Madulu wa kushoto mara baada ya kutembelea
kituo cha umsambazaji wa umeme kilichopo Mlandizi ikiwa ni ziara yake ya
kikazi yenye lengo la kukagua miradi ya nsihati ya umeme (PICHA ZOTE NA
VICTOR MASANGU)
…………………………………………………………………………..
NA VICTOR MASANGU, PWANI
VIJIJI vipatavyo 54 katika mkoa
wa Pwani ambavyo wananchi wake walikuwa katika hali ya sintofahamu
kutokana na kukaa gizani kwa kipindi cha muda mrefu hatimaye wanatarajia
kupata na kunufaika na nishati ya umeme wa uhakika ifikapo mwezi
machi mwaka 2018 baada ya kukamilika kwa mradi wa kusambaza umeme
vijiji (REA) awamu ya tatu.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu
Waziri wa wizara ya nishati Subira Mgalu baada ya kufanya ziara yake ya
kikazi ya siku moja katika Wilaya ya Bagamoyo pamoja na Wilaya ya
Kibaha mkoani Pwani kwa ajili ya kutembelea baadhi ya miradi ya REA
ambayo inatekelezwa kwa awamu ya tatu pamoja na kujionea changamoto
mbali mbali zinazowakabili.
Pia Magalu amesema kuwa lengo la
serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli
ni kuhakikisha inapeleka huduma ya uhakika kwa wananchi wake pamona na
maeneo mengine yenye kutoa huduma za kijamii na kubainisha kuwa
wanatarajia ifikapo mwaka 2021 vijiji vtote nchini view vimefikiwa na
huduma ya nishati ya umeme.
Aidha Naibu Waziri huyo
alipotembelea kituo cha uzalishaji wa umeme kilichopo maeneo ya Mlandizi
aliliagiza Shirika la ugavi wa umeme Tanesco kuhakikisha wanajipanga
vizuri ili kuweza kupunguza malalamiko ambayoyamekuwa yakitolewa na
baadhi ya wananchi kuunguza vitu vyao majumbani kutokana na tatizo
la kukatika katika umeme kila mara bila ya kutoa taarifa.
“Jamani viongozi wangu wa Tanesco
kumekuwepo na baadhi ya malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa na wateja
kuhusina na hii hali ya kukatika katika kwa umeme mara kwa mara bila ya
taarifa hali amabyo inasababisha wakati mwingine wananachi hao kuunguza
vitu vyao hivyo katika hili mimi nawaomba mbadilike na mlifanyie kazi
katika kuhakikisha lawama hizi zinaondoka kabisa na nina imani
mtalifanyia kazi,”alisema Mgalu.
Kwa upande wake Meneja wa Shirika
la ugavi wa umeme (Tanseco ) Mkoa wa Pwani Martin Madulu amesema kuwa
kukamilika kwa mradi huo wa REA awamu ya tatu utakuwa ni mkombozi
mkubwa katika suala zima la nishati ya umeme kwani wanatarajia
kuwafikiza zaidi ya wateja 5000, na kuongeza kuwa mradi huo umegharimu
kiasi cha shiingi bilioni 5.
Meneja Madulu aliongeza kuwa
lengo la Tanesco ni kuhakikisha kwamba wanaboresha zaidi huduma ya
nishati ya umeme hususan katika maeneo ya vijijini kwa lengo la kuweza
kuwafikia wananchi wengie ambao wataweza kupata fursa ya kutumia
nishati hiyo katika kuendeshea shughuli zao mbali mbali za kimaendeleo.
Mhandisi mkuu ambaye
anayesimamia miradi ya umeme wa vijijini (REA) katika Mkoa wa Pwani Leo
Mwakatobe amesema licha ya kujitahidi katika kunga miundombinu mipya
kwa ajili ya nishati hiyo wanakabiliwa na chanagmoto kubwa ya kuwepo kwa
baadhi ya wananchi kugoma kuhama kwa ajili ya kupata njia ya kupitsiha
mradi huo hivyo kuwapa wakati mgumu katika utekelazaji wa majukumu yao.
“Katika miradi hii ya kusambaza
umeme vijijini kwa kweli baadhi ya maeneo bado tunakabiliwa na
changamoto kubwa ya wananchi kuwa wagumu kupisha eneo kwa ajii ya kuweza
kupata njia ya kupitisha nishati ya umeme, hivyo inatupa wakat mgumu
sana katika kufanya kazi zetu na wengi wao wanadai fidia ya kulipwa
lakini katika maradi huu hauna fidia kitu kikubwa ni kutupa ushirikiano
katika kufanikisha zoezi hili,”alisema Mhandisi Mwakatobe.
KUKAMILIKA kwa mradi wa umeme
vijijini awamu ya tatu (REA) katika Mkoa wa Pwani utaweza kuvinufaisha
vijiji vipatavyo 154 ambavyo baadhi ya vingine vilishapatiwa umeme huo
katika awamu ya kwanza pamoja na ya pili.