Binagi Media Group
Mkutano wa
siku mbili wa Sekta ya uziduaji (Madini, Mafuta na Gesi) 2017 umeanza hii leo
Mjini Dodoma, ukishirikisha wadau mbalimbali ikiwemo asasi za kiraia, serikali
pamoja na wanasheria kutoka ndani na nje ya nchi.
Mkutano huo
unaoandaliwa na muunganiko wa asasi za kiraia nchini ambazo zinaangazia utawala
bora katika sekta ya uziduaji HakiRasilimali, umelenga kujadili sera, sheria na
mifumo ya uendeshaji katika sekta hiyo kwa manufaa ya jamii na taifa kwa
ujumla.
Akifungua
mkutano huo, Padri Steven Munga alisema sekta ya uziduaji ni chachu ya
maendeleo nchini hivyo inapaswa kuangaziwa vyema na hatimaye kuleta matokeo
chanya kwa taifa.
Mwenyekiti
wa Bodi ya HakiRasilimali, Donald Kasongi alisema mchango wa asasi za kiraia
katika sekta ya uziduaji ni mkubwa hivyo asasi hizo zinapaswa kushiriki na kushirikishwa
ipasavyo katika kuboresha sekta hiyo.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe alisema mkutano huo ni
ishara kwamba suala la kuboresha sekta ya uziduaji si la Rais John Magufuli
pekee bali pia asasi za kiraia kwani zina nafasi kubwa ya kuhakikisha
rasilimali zilizopo nchini zinabaki kuwa utajiri na siyo laana kwa taifa.
Washiriki wa
mkutano huo wametaka mazungumzo zaidi katika kuboresha sekta ya uziduaji nchini
ili kuhakikisha inatoa matokeo chanya kwa taifa badala ya kutumia manufaa ya idadi
kubwa ya wabunge bungeni kupitisha mikataba mibovu ambayo imeligharimu taifa.
Mgeni Rasmi, Padri Steven Munga akifungua mkutano huo
Mgeni Rasmi Padri Steven Munga (kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya HakiRasilimali, Donald Kasongi (katikati) pamoja na Mwanasheria Veronica Zano kutoka Zimbabwe (kushoto), wakiwa kwenye chumba cha mikutano baada ya ufunguzi wa mkutano wa uziduaji Mjini Dodoma
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe (kushoto) akizungumza na wanahabari kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa Bodi ya HakiRasilimali, Donald Kasongi (kulia) pamoja na Mwanasheria Veronica Zano kutoka Zimbabwe wakiwa kwenye mkutano huo
Mratibu HakiRasilimali, Rachel Chagonja kutoka akiwa kwenye mktano huo
Jenerali Ulimwengu ambaye ni mmoja wa watoa mada kwenye mkutano huo
Profesa Hamudi Majamba ambaye ni miongoni mwa watoa mada kwenye mkutano huo
Amani Mhinda ambaye ni mmoja wa watoa mada
Afisa Miradi kutoka shirika la HAKIZETU Jijini Mwanza, Gervas Evodius akifuatilia mkutano huo
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka Mwanza
Ashraf Omary ambaye ni Mkurugenzi wa shirika la METDO Tanzania akifuatilia mkutano huo
Washiriki mbalimbali wa mkutano huo
EmoticonEmoticon