Balozi
wa Norway nchini Tanzania kupitia kwa Balozi wake Balozi Bi.
Hanne-Marie Kaarstad leo wameweza kutiliana saini mkataba wa udhamini wa
donge nono la kiasi cha Dola 128200(USD) ambazo ni sawa na shilingi za
Kitanzania Milioni 300, ambazo zitaenda kusaidia Shirika lisilo la
Kiserikali la Busara Promotion kwa ajili ya tamasha la Sauti za Busara
2018.
Halfa
hiyo ya kutiliana saini imefanyika mapema leo Novemba 2,2017 katika
Ubalozi wa Taifa hilo la Norway, Jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na
wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari.
Awali
Mkurugenzi wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud alishukuru Ubalozi wa
Norway nchini Tanzania kwa kutoa udhamini huo ambao utasaidia uhai wa
tamasha hilo ambalo limejizolea sifa kwa muda mrefu.
“Sauti
za Busara imepata msaada, shukrani kwa ubalozi wa Norway nchini
Tanzania. Norway inaonyesha mfano mzuri wa kuigwa Duniani kwa kuchangia
katika maendeleio ya kudumu na mazingira rafiki. Kama ilivyo katika
malengo yake nchini Tanzania. Ubalozi wa Norway tangu mwaka 2009 unatoa
mchango mkubwa wa kifedha kwa shirika la Busara Promotions, ili
kuliwezesha kutimiza mpango mkakati wake hii ni pamoja na kusaidia
shughuli za kiutendaaji wa tamasha kwa kila mwaka na tunafurahia kwani
tunaamini utaendelea pia kwa mwakani” alieleza Mkurugenzi huyo Yusuf
Mahmoud.
Pia
akifafanua umuhimu wa tamasha la Sauti za Busara, Mkurugenzi huyo Yusuf
Mahmoud alibainisha kuwa, tamasha hilo limekuwa likiunganisha watu wa
rika na asili tofauti huku pia likiheshimu uhuru wa kujieleza sambamba
na kuleta umoja, Amani na kuimalisha jamii.
“Tamasha
la Sauti za Busara linatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sekta ya
muziki kukutana na kujifunza. Linaimarisha utaalamu katika sekta ya
Sanaa nchini hivyo yote haya lengo kuu la tamasha ili ni kuhakikisha
kutangaza amani, mshikamano na kuheshimu tamaduni tofauti” alimalizia
Yusuf Mahmoud.
Balozi
wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad akizungumza katika
tukio hilo mara baada ya kutiliana saini. Anayemfuatia ni Mkurugenzi wa
Busara Promotion, Yusuf Mahmoud na kulia ni Ofisa wa Busara Promotions.
Kwa
upand wake, Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad
ameahidi kuendeleza ushirikiano na Busara Promotions katika kusaidia
Sanaa na Utamaduni ambapo lengo kuu ni kukuza mashirikiano na
maingiliano ya kitamaduni kupitia sanaa hasa muziki katika jamii kwa
njia ya tamasha hilo la kila mwaka la Sauti za Busara.
“Najisikia
furaha sana katika siku ya leo katiliana saini udhamini huu mnono.
Tumekuwa na Busara Promotion kwa muda mrefu kuanzia 2008 mpaka sasa
tukiendelea kukuwa zaidi na kuleta mageuzi kwa jamii hasa kuleta mageuzi
makunwa sana kwa jamii ya Wazanzibar, Tanzania Bara na Ukanda wa
Afrika kwa ujumla.
Tunaamini
Sauti za Busara wamejijengea mizizi imara Visiwani Zanzibar na Tanzania
Bara kwa ujumla kupitia tamasha lao ambalo linainua na kulinda
utamaduni wa Mzanzibar huku pia likilinda hutu na utamaduni wake ndani
ya visiwa hivyo vya Zanzibar.” Alieleza Balozi Bi. Anne-Marie Kaarstad.
Balozi
huyo aliongeza kuwa, tamasha hilo pia limekuwa na nguvu kubwa ikiwemo
kukusanya watu wengi zaidi kutoka pande mbalimbali za Dunia na kukutana
mahala pamoja kufurahia.
Aidha,
Mkurugenzi wa Busara Promotions, Yusuf Mahmoud amebainisha kuwa, msimu
wa Sauti za Busara kwa 2018, tayari wametangaza listi ya wasanii na
vikundi ambapo jumla ya vikundi 20 kutoka Tanzania Bara, pia vipo kutoka
Afrika Kusini, Zimbabwe, DRC, Nigeria, Morocco, Algeria, Kenya,
Rwanda, Burundi, Malawi, Misri Sudan, Gambia.
Pia vipo vikundi kutoka nchi za Reunion, Norway, Denmark na Switzerland.
Katika
vikundi hivyo vinatarajia kuwa na Wasanii 400, ambapo wataonyesha uwezo
wao kwenye majukwaa matatu tofauti, shoo 46 zote zikiwa asilimia 100
‘live’ kwa siku nne mfululizo.
Pia
kutakuwa na mambo mbalimbali ikiwemo warsha na semina kwa wanamuziki wa
ndani na nje ambao watapata kubadirishana ujuzi na mbinu za kukuza
sanaa na masoko ya muziki wao.
Na Andrew Chale-MO BLOG, Dar e Salaam.
Mkurugenzi
wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud akizungumza katika tukio hilo.
Kushoto ni Balozi wa Norway nchini Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad
Mkurugenzi
wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud na Balozi wa Norway nchini
Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad wakitiliana saini udhamini huo mapema
leo Novemba 2, 2017. Wengine wanaoshuhudia ni maafisa kutoka Ubalozi wa
Norway na Busara Promotions.
Mkurugenzi
wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud na Balozi wa Norway nchini
Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad wakibadilishana hati walizotiliana
saini udhamini huo mapema leo Novemba 2, 2017.
Mkurugenzi
wa Busara Promotion, Yusuf Mahmoud na Balozi wa Norway nchini
Tanzania Bi. Hanne-Marie Kaarstad wakijibu maswali kutoka kwa wanahabari
(Hawapo pichani) mapema leo Novemba 2, 2017. ( PICHA ZOTE NA ANDREW
CHALE)
EmoticonEmoticon