SIDO TANGA YATOA MIKOPO YA ZAIDI YA BILIONI 1.6 KWA WAJASIRIAMALI MKOANI TANGA

February 20, 2025






Na Oscar Assenga,TANGA.

SHIRIKA la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) mkoani Tanga watoa mikopo ya zaidi ya Bilioni 1.6 kupitia MFUKO wa NEDF (National Entrepreneuship Development Fund) Kwa vikundi vya wajasiriamali mkoani Tanga katika Wilayani zote ili waweze kujikwamua kiuchumi.


Hayo yalisemwa leo na Meneja wa SIDO Mkoa wa Tanga Mhandisi Baliyo Christopher wakati akizungumza na gazeti la Nipashe ofisini kwake ambapo alisema pia mikopo hiyo ilitolewa kwa vikundi vya wajasiriamali Kwenye shughuli za uzalishaji mali ikiwemo usindikaji.


Alisema wengine ni wale wanaofanya shughuli za kuchakata mchonge,samaki pamoja na wanaozalisha bidhaa Mkoa huo ikiwemo karakana,gereji ambapo alisema mafanikio hayo yamepatikana Kwa kipindi cha miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu kuanzia machi 2021hadi June 2024.


Alisema mafanikio yaliyopatikana ni utoaji wa mikopo Kwa wajasiriamali wadogo wadogo 64 ambapo kiasi cha Sh.Bilioni 1.4 kilitumika kupitia wahisani kwa kushirikiana na Serikali pamoja na utoaji wa Mafunzo ya ujuzi kwa wajasiriamali ambapo walionufaika ni 1,450 wamepatiwa Mafunzo ya ujuzi mbalimbali .


Mafunzo hayo yaliwawezesha kuanzisha shughuli za kujiajiri na kuanzisha biashara ndogo ndogo mkoani Tanga ambapo wanawake 801 na wanaume ni 709 ambapo kiasi cha sh.Milioni 238,470,000 zilitumika kupitia Serikali na wahisani.


Meneja huyo Alisema pia walifanikiwa kutoa Mafunzo ya uendelezaji biashara Kwa wajasiriamali ambapo wanufaika wapatao 1,667 walipatiwa Mafunzo ya uendelezaji biashara mkoani Tanga ambapo wanaume ni 697 na wanaume ni 970 ambapo kiasi cha Milioni 85,050,00 zilitumika kupitia wahisani na Serikali.


Aidha alisema katika uboreshaji wa jengo la Mafunzo Kwa ajili ya wajasiriamali Serikali ilifanya ukarabati wa jengo la Mafunzo ya ujuzi lililopo katika mtaa wa Viwanda wa SIDO ambapo jengo hilo hutumika kuendeshea Mafunzo ya ujuzi ambapo kiasi cha Milioni 30,000,000 zilitumika ambapo Serikali iligharamia.


Akizungumza kuhusu ujenzi wa jengo la Viwanda Kwa ajili ya wajasiriamali ambapo jengo la Viwanda Kwa ajili ya wajasiriamali kutumika kwa ajili ya shughuli za Viwanda lipo katika hatua za umaliziaji huku Majengo hayo wajasiriamali hupanga Kwa nusu gharama za NHC za eneo husika Kwa mita mraba ambapo kiasi cha sh.MilionI 384,658,515.10 zilitumika ambazo zilitolewa na Serikali.


"Lakini pia wajasiriamali wamenufaika na Majengo ya Viwanda kwa gharama nafuu ambapo wajasiriamali 33 wamenufaika na Majengo ya Serikali Kwa kupanga Kwa gharama nafuu huku Viwanda hivyo vikiajiri ajira za kudumu 96 na ajira za muda 57 "Alisema


Aliongeza kwamba pia katika mafanikio mengine ni Idadi ya wajasiriamali waliofikiwa na huduma mbalimbali za SIDO kama vile Ushauri,Mikopo ,kutembelewa,kupata alama ya ubora,Mafunzo ,teknolojia na mashine,kuunganishwa na Taasisi mbalimbali na kadhalika.


"Ambapo katika jambo hili wajasiriamali 3,550 wamepatiwa huduma mbalimbali za kiujasiriamali kulingana na mpango biashara wa Mkoa ambapo kiasi cha Sh.Milioni 364,729,500 zilitumika na zilitolewa na Serikali pamoja na wahisani" Alisema.


Hata hivyo alisema pia walianzisha kituo cha ubunifu wa masuala ya Tehama (ICT INOVATION HUB) ambapo SIDO iliingia mkataba wa makubaliano na Tume ya Tehama ambapo mradi huo upo katika hatua za uandaaji wa mchoro wa jengo Hilo ambalo litakuwa ndani ya eneo SIDO -Gofu chini ambapo Serikali walishirikiana na Benki ya Dunia.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »