MHANDISI MTIGUMWE AIPONGEZA TWCC KWA KUENDELEZA BIASHARA ZA WANAWAKE WAJASIRIAMALI NA WAFANYABIASHARA TANZANIA

August 06, 2017

Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Methew Mtigumwe akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mhe Rukia Muwango alipotembelea banda la Chama Kikuu cha kuendeleza biashara za wanawake wajasiriamali na wafanyabiashara Tanzania (TWCC)

Na Mathias Canal, Lindi

Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Methew Mtigumwe amekipongeza Chama Kikuu cha kuendeleza biashara za wanawake wajasiriamali na wafanyabiashara Tanzania (TWCC) kwa kazi kubwa ya kuwaunganisha wanawake wafanyabiashara kutoka sekta zote.

Mhandisi Mtigumwe ameyasema hayo alipotembelea banda la TWCC wakati wa Maonesho ya Wakulima Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Msisitizo mkubwa alisema chama hicho kinapaswa kuwafikia wanawake wengi zaidi nchini wenye dhamira na ndoto ya kufanikiwa katika ujasiriamali na biashara ndogondogo na kubwa ikiwa ni sehemu ya kubaini fursa zilizopo kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi.

Alisema kuwa wawake wanatakiwa kuandaliwa kuwa na umoja wa kutetea haki na kukuza biashara zao kwa kutumia za mikakati nje na ndani ya nchi.

Mhandisi Mtigumwe aliongeza kuwa wanawake wanatakiwa kuwa na umoja, nguvu, sauti na mikakati ya pamoja yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kujikwamua kiuchumi na kijamii.

Mwanachama wa Chama Kikuu cha kuendeleza biashara za wanawake wajasiriamali na wafanyabiashara Tanzania (TWCC) ni mwanamke yeyote mjasiriamali anayemiliki kampuni au biashara iliyosajiliwa au kikundi, Taasisi binafsi, chama na vikundi, vya wanawake wafanyabiashara wa sekta yoyote.

Maonesho ya sikukuu ya wakulima Nanenane yanahusisha shughuli za wakulima, wafugaji wa mifugo, wafugaji wa nyuki, wavuvi, wanamazingira, wasindikaji wa bidhaa za mazao ya kilimo na mifugo, wizara taasisi/makampuni ya umma, makampuni binaf si, mabenki, Taasisi za umma na binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali.
 
Pia uzalishaji bora wa mazao ya nafaka, ubunifu wa teknolojia rahisi za kutotoa mayai, Kuongeza thamani ya mazao ya mifugo, Makampuni ya mawasiliano, ambapo Taasisi za elimu zitaonyesha ubunifu wa kumsaidia mfugaji, Tiba za asili, Wasindikaji wakubwa na wadogo wa mazao ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Asali, na Nta. 

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »