Bi. Joyce Msigwa ambaye ni Mratibu wa Faru Arts and Sports Development Organization (FASDO) akitoa maelezo kwa washiriki wa 'Bongo Style Competition' 2017, kuhusiana na asasi ya FASDO
Mwezeshaji Bw. Erick Chrispin akitoa semina kwa washiriki wa Bongo Style namna ya kujiongoza wenyewe katika maswala ya Fedha,Muda na uongozi.
Baadhi ya washiriki wa shindano la Bongo Style 2017, wakiwemo wapiga picha,waandishi wa miswada ya Filamu na wabunifu wa mitindo upande wa mavazi wakiwa wanafanya zoezi waliopewa na mwezeshaji Bw. Erick Chrispin (ambaye hayupo pichani)
Baadhi ya Washiriki wa Bongo Style Competition 2017 wakiwa wanafanya kazi waliyopewa na mwezeshaji Bw. Erick Chrispin (hayupo pichani) baada ya kumaliza semina yake.
Mkufunzi na Mtaalam wa maswala ya Picha Bw. Iddy John akitoa somo juu ya maswala ya picha kwa washiriki wa Shindano la Bongo Style kundi la Picha
Mbunifu maarufu wa Mitindo ya mavazi Martin Kadinda akitoa somo kwa washiriki kundi la mitindo
Washiriki wa kundi la Ubunifu wa mitindo upande wa mavazi wakipewa vitendea kazi.
Bi. Christina Pande(aliyesimama) ambaye ni Mtunzi na muongozaji wa Filamu, akiwapa darasa vijana ambao wapo katika kundi la Uandishi wa miswada ya Filamu shindano la Bongo Style 2017.
Picha zote na Fredy Njeje.
EmoticonEmoticon