Mkazi wa Bunju James Peter azoa milioni za Biko

May 14, 2017
Balozi wa Biko Tanzania Kajala Masanja akifurahia namba ya ushindi ambapo mkazi wa Bunju, jijini Dar es Salaam, James Peter amejinyakulia jumla ya Sh Milioni 10 katika droo iliyochezeshwa jana jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Emmanuel Ndaki. Picha na Mpiga picha wetu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MKAZI wa Bunju jijini Dar es Salaam, James Peter amefanikiwa kuibuka kidedea katika droo ya tano ya wiki ya kuwania Sh Milioni 10 baada ya kutangazwa mshindi kwenye kinyang’anyiro hicho.
Droo hiyo ya tano ya wiki imechezeshwa leo jijini Dar es Salaam na Balozi wa Biko, Kajala Masanja kwa kushirikiana na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Emmanuel Ndaki.
Akizungumza katika droo hiyo ya tano, Kajala Masanja alisema mshindi wa Milioni 10 wa wiki hii alibahatika kutangazwa mshindi baada ya kupigiwa simu mara tatu, huku mara mbili akishindwa kupokea simu kwa haraka.
Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akiagana na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Emmanuel Ndaki baada ya kumaliza kuchezesha droo ya tano ya Sh Milioni 10 ambapo mkazi wa Bunju, jijini Dar es Salaam, James Peter kutangazwa mshindi wa droo hiyo ambapo amejishindia jumla ya Sh Milioni 10.
Kajala Masanja akifurahia namba ya ushindi ya bwana James Peter
Alisema hata hivyo baadaye alipokea simu hali inayoonyesha kwamba alikuwa na bahati kubwa kwa kunyakua fedha hizo zinazotolewa kwa mshindi mmoja kila mwisho wa wiki, huku washindi wengine zaidi ya 20,000 wa zawadi za papo kwa hapo wakijishindia zawadi kem kem.
“Tumefanikiwa kumpata mshindi wa Sh Milioni 10 ambaye anatokea jijini Dar es Salaam, akiongeza idadi ya washindi wanne kutokea jijini hapa, huku mmoja pekee akitokea jijini Mwanza,” alisema Kajala.
Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven aliwataka Watanzania hususan wakazi na wananchi wa mikoa mbalimbali ya Tanzania kujitokeza kwa wingi kucheza biko ili waibuke washindi kwa kufanya miamala kwenye simu zao za Tigo, Vodacom na Airtel ambapo katika kipengele cha lipa bili wataingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na namba ya kumbukumbu 2456.
“Kucheza biko ni rahisi kwa saabubu baada ya kuweka kiasi kuanzia Sh 1000 ambayo inatoa ushindi wa papo kwa hapo pia humpa fursa mtu kuingia kwenye droo kubwa ya wiki ya kuwania Sh Milioni 10, huku zawadi za papo kwa hapo zinatolewa na Biko ikianzia sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, huku hadi sasa washindi zaidi ya 20,000 wakiwa wamenyakua zawadi mbalimbali za fedha kutoka kwetu Biko,” Alisema.
Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki alisema taratibu za uchezaji wa bahati nasibu ya Biko ni mzuri kwasababu unafuata sharia zote kutoka kwenye Bodi yao, huku akiwaondoa hofu Watanzania juu ya bahati nasibu ya Biko.
“Kila wiki ya droo ya Biko lazima tuwepo katika kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 10, hivyo nampongeza mshindi wa wiki hii na kuwatakia kheri wale wengine ambao wanafikiria kuingia katika tasnia ya michezo ya kubahatisha kwa sababu ni hatua nzuri kwa wachezaji wote,” Alisema Ndaki.
Baada ya kutangazwa mshindi, Biko inatarajia kukabidhi zawadi hiyo ya fedha nono kwa mshindi wao ambaye ni Peter mapema wiki ijayo kama walivyowapatia washindi wengine waliowahi kunyakua fedha hizo kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania hususan kwa mshindi wa Sh Milioni 10.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »