Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya vijana wenye umri
wa miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys imeanza mazoezi rasmi
leo Machi 12, 2017 kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Serengeti Boys itakuwa kambini Dar es Salaam hadi
Machi 26, mwaka huu ambako itakwenda Bukoba mkoani Kagera kwa ajili
ya mechi za kirafiki za kimataifa kujiandaa na michuano Afrika ambayo
sasa itaanza Mei 14, 2017 badala ya Mei 21, mwaka huu.
Michezo ya kirafiki ya kimataifa itakuwa ni dhidi
ya timu za vijana za Rwanda (Machi 28, 2017), Burundi (Machi 30, mwaka
huu) na Uganda Aprili 2, mwaka huu). Michezo yote itafanyika Uwanja
wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera.
Timu hiyo itarejea tena Dar es Salaam Aprili 3, mwaka
huu ambako siku inayofuata itaagwa kwa kupewa bendera na mmoja wa viongozi
wa nchi kabla ya kusafiri Aprili 5, mwaka huu kwenda Morocco kwa ajili
ya kambi.
Timu hiyo itaunganisha kwenda Cameroon Mei mosi,
mwaka huu ambako Mei 3, 2017 itacheza mechi ya kwanza na Cameroon kabla
ya kurudiana Mei 6, mwaka huu na siku inayofuata itakwenda Gabon.
Serengeti Boys ni timu ya vijana ambayo imefuzu kwa
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Gabon kuanzia
Mei 14, mwaka huu. Timu hiyo imepangwa Kundi ‘B’ pamoja na mabingwa
watetezi Mali, Niger na Angola. Ina lalengo ya kurejea
na Kombe la Afrika kwa vijana.
La ikitokea imekosa nafasi hiyo angalau ikafika nusu
fainali ambako kwa mafanikio hayo itakuwa tayari ina tiketi mkononi
ya kucheza fainali za Kombe la Dunia huko India, Novemba, mwaka huu.
Kikosi cha Serengeti Boys kinaundwa na Makipa: Ramadhan Kabwili, Samwel Edward
na Kelvin Kayego.
Walinzi: Kibwana Ally Shomari, Nickson
Kibabage, Israel Mwenda, Dickson Job, Ally Msengi, Issa Makamba na Enrick
Vitalis Nkosi.
Viungo: Kelvin Nashon Naftali, Ally
Ng’anzi, Mohamed Rashid, Shaaban Ada, Mathias Juan, Najim Mussa, Marco
Gerald, Abdulhamis Suleiman, Saidi Mussa na Cyprian Benedictor Mtesigwa.
Washambuliaji: Muhsin Malima Makame,
Yohana Mkomola, Ibrahim Abdallah, Assad Juma na Abdul Suleiman.
Benchi la Ufundi:
Bakari Shime (Kocha Mkuu)
Oscar Mirambo (Kocha Msaidizi)
Muharami Mohamed (Kocha wa makipa)
Kim Poulsen (Mshauri wa Ufundi)
Edward Evans (Mtunza Vifaa)
Shecky Mngazija (Daktari wa timu)
Gomez Dardenne (Mtaalamu wa saikolojia)
EmoticonEmoticon