MKURUGENZI MKUU REA APOKEA TUZO YA USHINDI WA REA SABASABA 2026

July 14, 2026




Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mha. Hassan Saidy, leo Julai 14, 2026, amepokea tuzo ya Muoneshaji Bora wa Taasisi za Serikali (Government Institutions Exhibitor), ambayo REA ilitwaa katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) 2026.


Tuzo hiyo imewasilishwa kwake na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma, Bi. Martha Chassama, kwa niaba ya watumishi walioshiriki katika maonesho hayo.


Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Mha. Saidy amewapongeza watumishi wa Wakala kwa juhudi, kujituma na ushirikiano wao ulioiwezesha REA kutwaa tuzo hiyo.


Aidha, amewataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi na ushirikiano katika kutekeleza miradi ya REA vijijini na vitongojini, ili kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanafikiwa na huduma za nishati na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.


Mwisho

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »