Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na mamia ya wananchi kabla ya kuzindua Mashindano maarufu ya Nage Mapinduzi Cup katika Viwanja vya Matumbaku, Wilaya ya Mjini, Unguja, Zanzibar. Mashindano hayo yanawahusisha wasichana kutoka majimbo mbalimbali ya mjini humo yameandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwakani.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Chama cha Kuweka na Kukopa (Vicoba-Together) katika sherehe iliyofanyika Skuli ya Chekechea, Miembeni, Zanzibar. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Unguja. Masauni alikichangia chama hicho shilingi milioni tatu.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimkabidhi Mkurugenzi wa Redio ya Coconut mjini Unguja, Zanzibar, Ally Dai, jezi kwa ajili ya Mashindano maarufu ya Nage Mapinduzi Cup ambayo yamezinduliwa na kiongozi huyo katika Viwanja vya Matumbaku mjini humo. Mashindano hayo yanawahusisha wasichana yameandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwakani.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto aliyevaa kofia) akiyapokea Maandamano ya timu 38 za Mashindano ya Nage Mapinduzi Cup katika Viwanja vya Matumbaku, Wilaya ya Mjini, Unguja, Zanzibar. Mashindano hayo yanawahusisha wasichana kutoka majimbo mbalimbali ya mjini humo yameandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwakani.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wanachama wa Chama cha Kuweka na Kukopa cha Vicoba-Together (hawapo pichani) kabla ya kuzindua kikundi hicho katika sherehe iliyofanyika Skuli ya Chekechea, Miembeni, Zanzibar. Kushoto ni Katibu wa Vicoba Together, Mwashum Mohammed Mustafa. Kulia ni Katibu wa Jimbo la Kikwajuni, Kassim Ally Juma.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni akizikagua timu ya Kikwajuni na Baa kutoka Jimbo la Mtoni kabla ya kuanza Mashindano ya Nage Mapinduzi Cup katika Viwanja vya Matumbaku, Wilaya ya Mjini, Unguja, Zanzibar. Mashindano hayo yanawahusisha wasichana kutoka majimbo mbalimbali ya mjini humo yameandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwakani.
Mchezaji wa Timu ya Kikwajuni, mjini Unguja, Zanzibar akijaza chupa mchanga wakati wa Mashindano ya Nage Mapinduzi Cup katika Viwanja vya Matumbaku, Wilaya ya Mjini, Unguja, Zanzibar. Mashindano hayo yanawahusisha wasichana kutoka majimbo mbalimbali ya mjini humo yameandaliwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mwakani. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni alizindua Mashindano hayo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa Chama cha Kuweka na Kukopa cha Vicoba Together. Masauni alikichangia chama hicho shilingi milioni tatu. Picha zote na Felix Mwagara
EmoticonEmoticon