Dar es Salaam Novemba 1, 2016. Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidijitali ya Tigo Tanzania leo imewatambulisha washindi 16 wa shindano la Tigo Fiesta Super Nyota lililofanyika katika mikoa 15 ya Tanzania Bara. Shindano hilo lililoratibiwa na Kampuni ya Prime Time Promotions liliendeshwa katika mikoa hiyo kwa kipindi cha miezi miwili na nusu. Mshindi wa fainali yake atajulikana wakati wa fainali ya mwisho Novemba 5, 2016 itakayofanyika jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika mkutano wa vyombo vya habari wakati wa kutangaza washindi hao, Mratibu wa mradi wa Tamasha la Fiesta 2016 kutoka Tigo, Balla Shareeph alisema, “ Tigo inaona fahari kuinyanyua sekta ya muziki ya Tanzania kwa kuwapatia wasanii wanaoibukia jukwaa la kuonesha vipaji vyao waweze kufikia kiwango cha juu nchini na wakati huo huo kuwawezesha kutambuliwa na chapa mbalimbali za muziki.”
Shareeph aliwapongeza washindi kwa kutumia nafasi hiyo kuwakumbusha wao wenyewe pamoja na umma kwa ujumla kwamba wanaweza kupata tiketi zao kwa ajili ya fainali hiyo ya kuhitimisha tamasha la Fiesta 2016 ambalo litafanyika katika viwanja vya Leaders Novemba 5, 2016 kwa kutumia mtandao wa Tigo Pesa.
Shareeph alifafanua, “Ili kupata tiketi kupitia Tigo Pesa wateja wote wa Tigo na wasio katika mtandao huu wanatakiwa kulipia tiketi kwenda namba 0678 888 888. Mkakati huu unalenga kuwapatia Watanzania njia ya kawaida na rahisi ya kupata tiketi zao.”
Washindi Super Nyota 16 ambao majina yao ni Nchama Anton a.k.a Nchama, Raphael Charles Manengo a.k.a Manengo kutoka (Mwanza), Ibrahim Juma a.k.a Mpanduji(Shinyanga) , Obed Moses a.k.a O strings(Muleba), Salum Asman a.k.a Alinacha ( Kahama), Gasper Festo a.k.a YOW (Tabora) Alex Joseph .a.k.a TIZO( Singida), Godfrey Andrew Mhoja a.k.a NEXUS( Dodoma) Hamad Hussein a.k.a Med Botion (Morogoro) Cyril Henry Isidor a.k.a So Real(Tanga) Wilson Pascal a.k.a Willy Desmiller( Mtwara ) Charles Mariki a.k.a Gerere(Moshi) Mohammedy Amiry a.k.a Croozy (Arusha), Amina Chibaba a.k.a Ammy Chiba (Mbeya) Leonard John Haule a.k.a sauti classic (Sumbawanga) wata zawadiwa simu ya kisasa ya Tecno Y3+ Music, ikiwa na muda wa maongezi.
Katika mkutano huo ambao ulihudhuriwa pia na Mratibu wa shindano la Super Nyota chini ya mrengo wa Tamasha la Fiesta 2016, Nickson George ambaye alisema, “Tunayofuhara kubwa kutangaza kwamba washindi 16 Super Nyota ambao watashiriki katika Fainali Kuu ya Fiesta 2016. Tunatarajia kuendelea kishukuru jamii kwa kuandaa shindano kama hili katika kuinyanyua sekta ya muziki na burudani ndani ya Tanzania.”
Tamasha ya Tigo Fiesta 2016 ni tukio linaloendeshwa kwa ubia baina Kampuni ya Prime Time Promotions na Tigo Tanzania na wakati huo huo Tigo ikiwa ndio mdhamini mkuu.
EmoticonEmoticon