WILAYA YA HAI WAZINDUA KAMPENI YA KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA UJENZI WA MADARSA KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

October 25, 2016
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Said mecky Sadiki akishiriki katika uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya msingi Msamadi ,uchimbaji ulioenda sanjari na uzinduzi rasmi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya ya Hai.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akishiriki kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya msingi Msamadi iliyopo wilayani Hai.
Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Hai,Juliet Mushi akishiriki kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzo wa madarasa matatu katika shule ya msingi Msamadi iliyopo wilayani Hai.
Baadhi ya wananchi wakishiriki katika uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Msamadi.
Msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Msamadi ukiwa umechimbwa na wananchi wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule zilizoko wilaya ya Hai.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiki akizungumza wakati akizindua rasmi kampeni za kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya ya Hai.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akizungumza na wananchi juu ya wazo la kuanzishwa kwa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya ya Hai.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa wakinyanyua mikono kuashiria kuunga mkono kampeni hiyo.
Diwani wa kata ya Masama Kusini Elingaya Masawe (Chadema) akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa madarasa katika shule za msingi na sekondari wilayani Hai.
Diwani wa kata ya Bomang'ombe ,Joe Nkya (Chadema) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa uliofanyika katika shule ya msingi Msamadi wilayani Hai.
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hai na Diwani wa kata ya Machame Magharibi Goodluck Kimaro (Chadema) akizungumza katika uzinduzi huo.
Mkuu wa wilaya akizungumza namna wanavyoshirikiana na Madiwani wa upinzani katika shughuli za menedeleoo ya wananchi wilayani Hai.kulia kwake ni Diwani wa kata ya Masama Mashariki ,John Munis (Chadema).

Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akitoa maelezo juu ya namna wananchi watakavyo changia katika ujenzi wa madarasa kwa njia ya harambee ili kupunguza changamoto ya vyumba vya madarasa katika wilaya ya Hai.
Baadhi ya wananchhi waliofika katika uzinduzi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa wakitoa ahadi zao wakati wa harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi huo.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akiongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Msamadi iliyopo katika kijiji cha kwa sadala.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Swissport wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyojiri wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Ujenzi wa vyumba vya madarasa ukiendelea katika shule ya msingi Msamadi iliyopo kijiji cha Kwa Sadala wilayani Hai.
Mafundi ujenzi wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadiki pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Swissport.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Swissport wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiki pamoja na Mkuu wa wilaya ya Hai ,Gelasius Byakanwa mara baada ya kumalizika kwa harambee ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa ambapo Swissport wametoa kiasi cha Sh Mil 15. 

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »