*📌Asisitiza watumishi wa Tanesco kuongeza juhudi katika utendaji wa kazi ili kuvifikia vipaumbele vya Serikali*
📍Dodoma
Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, ameongoza kikao kazi cha Watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Jijini Dodoma.
Mhe. Ndejembi ameeleza kuwa lengo la kikao kazi hicho ni kujadili utekelezaji wa majukumu ya Shirika, kupanga mikakati ya kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja, lakini pia kufanya tathmini ya utendaji kazi na kuweka mikakati mipya ya kuongeza kasi ya utoaji huduma bora.
Naye, Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Salome Makamba amesema kikao hiki ni muhimu kwasababu tunaona dhamira yako Mhe. Waziri wa Nishati ya dhati ya kupeleka huduma bora kwa wananchi wa Tanzania hususani yale maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hii.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mha. Felchesmi Mramba amemshukuru sana Waziri wa Nishati Mhe. Deogratius Ndejembi kwa kuitisha kikao kazi hicho na Watumishi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) a kuwapongeza kwa kutoa huduma bora kwa Wateja wake .
Naye, Balozi Zuhura Bundala Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) amemshukuru sana Waziri wa Nishati Mhe. Deogratius Ndejembi kwa kuhudhuria kikao kazi hicho amesema bodi inamuhakikishia kuwa shirika Lina wataalamu wa kutosha kwa ajili ya utekelezaji ili kuleta matokeo makubwa.
Akizungumza kwenye kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bw. Lazaro Twange ameeleza kuwa wao kama shirika wanahusika na Uzalishaji wa Umeme, Usafirishaji wa Umeme pamoja na Usambazaji wa Umeme kwa wateja na kuongeza kuwa, kwasasa kuna miradi 41 inayofadhiliwa na Serikali ya Tanzania lakini pia Wahisani wa Maendeleo, na kupelekea kuwa Jumla ya gharama za miradi hiyo kufikia takriban ya trilioni 13.4
Sambamba na hilo Shirika la Umeme Tanzania linazalisha MW 3,807.69 sawa na asilimia 93.47 za umeme huku Makampuni binafsi yakiwa na MW 266.01 sawa na asilimia 6.53 za umeme.
‘’Sisi kama Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) tumejipanga ndani ya siku mia moja kutekeleza miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufunga Transfomer mpya 500, lakini pia ufungaji wa mita Janja (Smart meter) 200,000 kwa wateja’’. Ameeleza Twange.
#NishatiTupokazini.








EmoticonEmoticon