DIWANI ATAKA MSHIKAMANO NDANI YA VIKOBA

March 03, 2016




Tangakumekuchablog
Korogwe, DIWANI wa kata ya Kerenge halmashauri ya Korogwe mjini, Shebila Said Shebila (CCM), amewataka wanachama wa Vikoba Upendo Tupendane cha Mazinde Tarafa ya Mombo kushikamana na umoja wao na kuyafikia malengo waliyojiwekea.
Akizungumza katika mkutano mkuu wa wanachama wa vikoba Mazinde jana, Shebila alisema umoja huo ni mfano kwa wanawake wengine kujiunga kwani mbali ya maendeleo waliyopata pia wamekuwa chachu ya maendeleo Mombo.
Ameitaka Serikali kutuma wataalamu wa elimu ya vikoba ili wakulima na wajasiriamali wa kazi za mikono kujiunga na kuweza kufaidika na mikopo ya kukopa na kulipa.
“Kabla ya kuja hapa nilikuwa nazisikia sifa zenu na najua nini mumefanya na leo mumesimama hapa, kwa jitihada zenu na umoja wenu nina imani kila mmoja hapa baada ya mwaka mmoja atakuwa ni tajiri wa mfano” alisema Shebila na kuongeza
“Muko wanachama zaidi ya mia na ukiangalia kuna wengine wanajiunga huu ni mtaji tunaoweza kusema jiunge utajirike hongereni sana” alisema
Diwani huyo amevishauri vikundi hivyo kuwa wabuni miradi mengine zaidi na halmashauri itawasaidia kwa hali na mali kuhakikisha unakomesha umasikini majumbani.
Alisema Tarafa ya Mombo vijijini vya Mazinde viko na rasilimali nyingi za kujikwamua na umasikini kikiwemo kilimo cha matikiti maji na zao la mkonge hivyo kujiunga na vikundi ni njia rahisi kujipatia fursa za mikopo.
Kwa upende wake wa Kikoba Tupendane, Issa Sigge,  amemtaka diwani huyo kupata asilimia 20 ya halmashauri kwa vijana na vikundi ili kuimarisha vikundi vyao na kupunguza wimbi la watu wasio na kazi.
Alisema kuna vijana wengi wamekaa bila kazi ya kufanya hivyo kuipata asilimia hiyokuanweza kuwavutia vijana na kuondosha wimbi la wasio na kazi Mazinde jambo ambalo litawasukuma katika kazi za ujasiriamali.
“Mhshimiwa diwani hebu katupigie chapuo kule katika mabaraza yenu ya madiwani kuipata ile asilimia 20 ya halmashauri, hii itawasukuma vijana na wasio na kazi kujiunga na vikundi” alisema Segga
Segga aliwataka wanachma wa vikoba kudumisha umoja na mshikamano ili kuweza kuyafikia malengo yao na kuhakikisha kila mwanachama anawasilisha michango yake kwa wakati.
                                          

 Wanachama wa Vikoba Tupendane Mazinde Wilayani Korogwe Mkoani Tanga wakionyesha pesa walizochanga wakati wa mkutano mkuu wa Umoja huo uliofanyika Mazinde jana. Jumla ya shilingi milioni moja laki mbili zilichangwa.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »