NA OSCAR ASSENGA, TANGA.
MWENYEKITI wa Klabu wa Coastal Union ya Tanga,Hemed Aurora
amesema baada ya kumalizika Ligi kuu ya Vodacom watatangaza muda wa kutoa za
uanachama wa klabu hiyo kwa mtu yoyote anayetaka kuwa mwanachama lakini sio
kikundi kutokana na katiba yao
inavyosema.
Kauli hiyo inatokana na malalamiko yaliyotolewa na wapenzi cha timu hiyo iliyoyatoa kwenye kikao
chao na waandishi wa habari jana kuelezea masikitiko yao ya kuzungushwa kupewa kadi za uanachama bila
sababu za msingi kwa kipindi cha miezi miwili.
Akizungumza kwenye mkutano huo, wapenzi hao ambacho
kilifanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Splended na kuhudhuriwa na wapenzi hao
ambao wanajiita Coastal Asili ,Kiongozi wa wapenzi hao,Abdullatif Omari Famau alisema
wanakaribu miezi miwili wamekuwa wakifuatilia suala la kadi bila kumkuta katibu
wa klabu hiyo,Kassim El Siagi.
Katika maelezo yake,Famau alieleza kuwa Kutokana na hali
hiyo wakaamua kumfuata katibu huyo nyumbani kwake kwa sababu kuna watu ambao
walikwenda nyumbani kwake na kufanikiwa kupewa kadi hizo nao wakaona watumie
njia hizo kwa sababu katibu anakaa na vitu vya klabu.
Alisema baada ya kutokea hali hiyo waliamua kumpigia simu
Katibu huyo ambaye aliwajibu kuwa kadi za uanachama za klabu hiyo simesitishwa
kutolewa kwa sababu klabu hiyo inataka kuingiliwa na watu ambao ni wavamizi ambao
wanataka kuiharibu timu hiyo hivyo wao hawatakubali
Baada ya kutokea hali hiyo waliamua kuunda kundi hilo ambalo wamelipa jina
la wapenzi wa Coastal Union ambao lengo lao ni kutaka kupatiwa kadi na waliamua
kwenda nyumbani kwake na kumkuta mkewe na kumuachia maagizo ambapo baadae
katibu aliwapigia ujumbe kwenye simu akiwaambia wasipeleke magenge nyumbani
kwake kwa sababu hapendi mambo ya klabu yafike nyumbani kwake.
Kutokana na hali hiyo waliamua kuandika barua yenye nakala
tatu ambazo zilipelekwa Chama cha soka
Mkoa wa Tanga TRFA,Chama cha soka wilaya ya Tanga TDFA na kwa katibu wa Coastal
Union lengo la barua hiyo ilikuwa ni kumuomba katibu huyo kuwa muwazi ni lini
fomu za uanachama zitakuwa tayari lakini mpaka leo hawajapata majibu
Hivyo hali hiyo iliwapelekea wanachama hao kujiunga pamoja
na kuchora mabango na kupita nayo kwenye mechi yao na Kagera Sugar ambayo
yalikuwa yana ujumbe tofauti tofauti ambapo baadhi yao yalikiwa yakisomeka
“Uongozi wa Coastal Union umefeli” Kadi za uanachama wa Coastal Union ni haki yetu na Mwenyekiti
fanya kazi na wajumbe na sio wapambe.
Alisema wao watakwenda klabu Jumatano kuangalia kama suala
la ujazaji wa fomu hizo zitakuwa likifanyika kama
waliyoelezwa na Mwenyekiti huyo lakini akasema kuna baadhi ya watu waliokwenda
kwa uongozi huo na kutoa pesa na kupewa kadi bila kujadiliwa .
Binafasi wakati tunafuatilia jambo hilo la kadi walichukua katiba ya Coastal
Union na kuingalia wakaelewa sifa za mwanachama na wengi wao wakawa na sifa
hizo lakini bado katibu huyo akawa mzito kutoa kadi hizo.
Alisema endapo watashindwa kupatiwa fomu za uanachama
watawashtaki kwa shirikisho la soka nchini TFF kwa kuanzia ngazi za chini kwa
sababu wao walifuata utaratibu mzuri ili kuweza kupata kadi hizo za uanachama.
Aurora alisema wao
waliwaambia wapenzi hao wasubiri mpaka ligi itakapomalizika ndio wapewa fomu za
uanachama kwa mtu mmoja mmoja na sio kwa kundi ambao watapewa kadi za uanachama
na kujaza baadae wajadiliwe kwa mujibu wa katiba yao na hawana matatizo na mtu yoyote
Alisema lakini kitendo ambacho kimefanywa na wapenzi hao
kwenye mechi hiyo kuigawa timu hiyo na kuwadhalilisha uongozi kimewaumiza sana kwani ishara hiyo
inaonyesha kuna mpasuko jambo ambalo sio la kweli.
Alisema hivi sasa hawawezi kulumbana na wapenzi badala yake
wanafanya matayarisho kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu simu
ujao ikiwemo mikakati mingine ya kuipa maendeleo timu hiyo na sio vyenginevyo.
Akizungumzia suala la mabango,Meneja wa timu hiyo,Akida
Machai alisema yenye anafikiri suala hilo
limetokana na uongozi wa klabu hiyo kurekebisha makosa yaliyopo kwenye timu
hiyo ikiwemo kuacha kuvaa jezi za kampuni ya sound ambazo walikuwa wakizivaa
zamani bila faida yoyote ndani ya miaka miwili na nusu.
Machai amesema malumbano hayo yote yanayokana na wao
kubadilika na kuacha kuvaa jezi hizo na badala yake hivi sasa wamepata mdhamini
mpya wa kiwanda cha Pembe ambaye wanamtumia hivyo hata jezi zao zimeandikwa
jina la Pembe.
“Wadhamini wetu
waliopita walikuwa wababaishaji kutokana na hawakuwa na manufaa yoyote kwetu
hivyo sasa tumebadilika ndio chanzo cha kuleta hali hiyo ndani ya timu hiyo
“Alisema Machai.
Kwa upande wake,Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa timu
hiyo,aliupongeza uongozi huo kwa manufaa makubwa ambayo wameyaleta kwenye timu
hiyo ambayo hapo awali hayakuwepo lakini anashangazwa na kitendo cha mashabiki
wanaotaka kuivuruga.
EmoticonEmoticon