NA OSCAR ASSENGA ,KOROGWE.
MWENYEKITI wa Jumuiya wa
Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Arusha,Robinson Meitinyiku
amesema haoni umuhimu wa kuwepo serikali tatu badala yake watanzania
washikamane kuhakikisha zinapatikana serikali mbili ili waweze kudumisha
muungano uliochwa na waasisi wa Taifa hili hayati Julius Kambarage Nyerere na
Abeid Amani Karume.
Meitinyiku aliyasema hayo
juzi wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Hale Mkoani Tanga baada ya
kumalizika mbio za pikipiki za uzalendo zilizofanywa na Jumuiya ya Umoja wa
Vijana Taifa ambazo zinakwimbizwa nchi
nzima zikiwa na lengo la kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara
na Tanzania Zanzibar
Alisema serikali tatu itakuwa na madhara makubwa ikiwemo
kuwaongezea watanzania gharama za uendeshwaji wake,kuigawa nchi yetu pamoja na
kuudhofisha muungano ambao ndio nguzo kuu iliyowachwa na viongozi waliowahi
kuliongoza Taifa hili.
Meitinyiku ambaye pia ni Mratibu
wa mbio za Pikipiki Kanda ya Kaskazini alisema watanzania walitegemea uchaguzi
uliofanywa kwa Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph
Warioba na Rais wa Jakaya Kikwete kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba
ungeleta tija na mafanikio kwa sababu ya nyadhifa ambazo aliwahi kuzishika kwa
Taifa hili badala yake anataka kuwaangamiza watanzania kwa kutaka serikali
tatu.
“Tuna mshangaa sana Jaji Warioba kama alitaka serikali tatu
basi angesema tokea kipindi kile akiwa waziri mkuu na sio wakati huu“Alisema
Meitinyiku akisisitiza serikali tatu ni sawa na kuwaletea matatizo watanzania.
Aliongeza gharama za serikali
ya tatu zitapatikana wapi kutokana na kutokuwa na vyanzo vya kuingizia mapato
hivyo kutaka fedha ambazo zingeweza kutumika kwenye matumizi hayo ni bora
zingetumika kuongeza maendeleo ya nchi.
“Tutasema kweli fitna kwetu
mwiko….nawaambieni tukiomuonea haya Warioba wakati huu atatuangamiza watanzania
lazima tuwe na umoja ili kuweza kupinga serikali tatu kwa nguvu zote “Alisema Mwenyekiti
huyo.
Aidha alisema hakuwahi kuona
nchi ikiitwa Tanganyika kama
Warioba anasema hilo linawezekana basi yenye na
familia yake waende wakaishi ziwa Tanganyika ili aweze kutimiza
malengo yake na sio watanzania.
Hata hivyo alisema watanzania
wanamshukuru Mwenyekiti wa tume ya Katiba kwa aliyowafanya lakini kwa suala la
serikali tatu hawatakuwa tayari kumuungano mkono hata kidogo.
Alisema tukiongeza
serikali ni dhahiri kuwa kutakuwa na
kizazi kijacho ambacho hawataweza kusoma hivyo lazima tumuenzi mwalimu Nyerere
kwa kuendelea kudumisha serikali mbili ambazo zitaleta maendeleo.
Alieleza kuwa wakati umefika
sasa kumtetea Rais Kikwete kwa rasimu aliyoianzisha kwa nia njema aliyokuwa
nayo ya kuwapatia watanzania katiba mpya lazimi viongozi walioteuliwa
kuisimamia wanataka kumuyumbisha.
“Jaji Warioba amestaafu alipopewa kazi
hiyo alionekana anaweza kuifanya lakini kumbe anataka kuharibia hivyo
anaangaliwe kiumakini ili asije akalitia taifa kwenye janga kutokana na
misimamo yake ya kutaka kuudhofisha serikali mbili “Alisema Mwenyekiti huyo.
Awali akizungumza,Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Mkoa wa Tanga,Abdi Makange alisema jumuiya hiyo
popote pale watasimama imara kupigia debe serikali mbili kwa sababu wanaotaka
tatu ni waroho wa madaraka.
Makange alisema viongozi wanaotaka serikali tatu wanataka
kulisababishia taifa hili machafuko na hiyo itakuwa ni dhahiri kuwagawa
watanzania ambao wanaendelea kuienzi tunu ya amani walioachiwa na waasisi wetu.
“Serikali ya tatu
ardhi yake itapatikana wapi ?mapato yake yatapatikanaje tusikubali kabisa kwani
wanaotaka hivyo hawana nia njema nasi bali watatusababishia machafuko .
Kwa upande wake,Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa
aliipongeza Jumuiya ya Umoija wa Vijana Chama cha Mapinduzi kwa kuamua
kuendesha mbio hizo za uzalendo.
EmoticonEmoticon