TAASISI YA BRIEN HOLDEN KUZINDUA HUDUMA YA UPIMAJI MACHO NA UTOAJI MIWANI KWA GHARAMA NAFUU

April 03, 2014

 
Ofisa Mkazi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Brien Holden Vision, Eden Mashayo akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam jana kuhisina na uzinduzi wa upimaji macho utakao fanyika Dar es Slaam free market mkabala na kituo cha DSTV , Kinondoni jijini Dr es Salaam. Kushoto ni Mratibu mradi huo Violet Shirima.
 Ofisa Mkazi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Brien Holden Vision, Eden Mashayo akionesha miwani itakayozinduliwa.
********
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa utoaji wa huduma ya macho bure, itakayofanyika Dar es Slaam free market mkabala na kituo cha DSTV , Kinondoni jijini Dr es Salaam.

Ofisa Mkazi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Brien Holden Vision, Eden Mashayo alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema wameamua kutoa huduma hiyo bure kwa sababu inakadiriwa, watanzania Milioni 3.5 wameathirika na ugonjwa wa macho wengi wao ni  wenye umri wa miaka 40 na kuendelea.

Alisema huduma hiyo itaanza kutolewa leo hadi Aprili 11 mwaka huu jijini Dr es Salaam, kuhamasisha watu kuwa na desturi ya kupima macho mara nyingi zaidi.

 ‘’Tumeandaa miwani za aina 12 ambazo saizi zote zinapatikana na tutaziuza kwa bei nafuu kuliko wanavyouza mawakala wengine’’ alisema Mashayo.

Aliongeza kuwa Taasisi hiyo inatoa huduma katika mikoa nane ambayo ni Mbeya, Mwanza, Mtwara, Singida, Iringa, Dodoma, Songea na Lindi. 

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »