NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Luteni
Mstaafu,Chiku Gallawa amesema mkoa huo umepanga kuongeza upatikanaji wa huduma
ya maji safi na salama kufikia asilimia 65 vijijini na mijini 75 ifikapo mwaka
2015 katika maeneo mbalimbali mkoani hapa.
Gallawa alitoa kauli hiyo
hivi karibuni wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema
upatikanaji wa maji kwa mkoa hadi kufikia octoba 2013 vijijini ilikuwa ni
asilimia 46,Tanga Jiji ilikuwa ni asilimia 91,Korogwe mji asilimia 65 na miji
midogo iliyobaki ilikuwa ni asilimia 39.
Akizungumzia mpango wa
kutekeleza matokeo makubwa sasa mkoa wamepanga kujenga miradi ya maji kwenye
vijiji 100 hadi kufikia Juni 2014,kujenga vituo (vitalu)2,831 vya maji kwenye
vijiji hivyo 100 hadi kufikia kipindi hicho.
Alisema pamoja na hayo
wamepanga kuunda vyombo vya watumiaji maji COWSOs(Community Owned Water Supply
and Sanitation Organisations)815 hadi kufikia mwezi Juni 20 ambapo mpango huo
unatekelezwa kwenye vijiji 10 kwa kila halmashauri.
Alivitaja vijiji ambavyo
vilivyopewa kipaumbele na miradi hiyo ,kwenye halmashauri kumi ambapo Handeni ni Pozo,Misima,
Kibaya,Kwamsangazi, Msilwa,Kwaluwala,Msanje, Gole, Kilimilang’ombe, Malezi,
Kwandungwa na Manga ambapo vijiji ambavyo miradi hiyo imekamilika ni Misima(bwawa
1 limejengwa na Tanzania Japan Food Aid Counterpart wakati Mkata mradi huo pia
umekamilika.
Aliongeza vijiji vyengine
kwenye halmashauri hiyo kuwa ni Hoza,Komkonga ,Kwanyange,Mkata na Komnara
ambayo vilinufaika na mradi huo ambao utapunguza adha ya huduma hiyo kwao.
Alisema halmashauri nyengine
ni Kilindi ambapo vijiji hivyo ni Mafisa,Mgera,Muungano, Kilindi,Mswaki,
Balang’a,Jungu,Negero,Kimbe, Chamtui,Kwediboma,Mafuleta, Kikunde,Saunyi na
Kwekivu wakati kwa halmahauri ya Korogwe mji, ni Kwamsisi,Kwakombo,Kwamndolwa, Kwameta,
Mahenge,Kwasemangube, Lwengera,Relini,Mgombezi, Mgambo na Msambiazi.
Kwenye halmashauri ya Korogwe
vijijini ni Mwenga,Mlembule,Hale, Mnyuzi,Vugiri,Kwamkole, Changalikwa,Mashewa,Makumba
na Kwashemshi ambayo tayari miradi iliyofanyika kwenye vijiji vya foroforo
vilula nane,walei vituo kumi na nane na lewa vituo vipatavyo kumi na tano.
Aidha alizitaja halmashauri
nyengine ambazo zinanufaika na mradi huo ni Muheza ambapo vijiji vya
Kibanda,Nkuba,Kwemkohi, Kisiwani,Ubembe,Misongeni, Mikwamba,Kigogo
Mawe,Kivindo,Kilongo na Mlingano huku miradi iliyokamilika mpaka mwezi desemba
ilikuwa ni vijiji vya Misongeni,Mikwamba na Kigongo-Mawe.
Aliongeza kuwa katika
halmashauri ya Jiji la Tanga vijiji ambayo vinatarajiwa kunufaika na mradi huo
kuwa ni
Mwarongo,Kirare,Mapojoni, Marungu,Geza,Mpirani, Chongoleani,Ndaoya,Kibafuta na
Mleni wakati kwenye halmashauri ya Mkinga vijiji vya Mapatano,Daluni
Kibaoni,Bamba Mwarongo,Doda, Kichalikani,Kilulu Duga,Palungu
Kasera,Mwakijembe,Mbuta na Bwagamacho.
Aliita halmashauri ya wilaya
ya Lushoto kuwa ni
Irente,Mlola-Lwandai,Ngulu, Mlalo-Mwangoi,Shume,Gologolo, Madala na Kivingo
wakati Irente na Mwangoi-Mlalo miradi hiyo imeshakamilika.
Hata hiyo alisema kwenye
halmashauri ya wilaya ya Pangani miradi hiyo inatekelezwa kwenye vijiji vya
Mwera,Kigurusimba,Mzambarauni, Mikocheni,Kimang’a,Madanga, Kwekibuyu,Bweni,Masaika
na Stahabu huku halmashauri ya Bumbuli miradi hiyo ikiendeshwa Bumbuli, Kweminyasa, Mgwashi, Kwalei, Kwadoe,Kwekitui
na Soni wakati miradi iliyokamilika tayari ni Bumbuli na Kweminyasa.
Mwisho.
EmoticonEmoticon