matukio katika picha kamati za Bunge maalum la Katiba
Spika
Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Pius Msekwa (kulia)
akitoa ufafanuzi leo mjini Dodoma kuhusu hati ya Muungano kwa wajumbe
wa Kamati namba mbili(2) ya Bunge Maalum la Katiba baada ya wajumbe hao
kumuomba aende kuwaelimisha juu ya hati hiyo. Wengine ni Mwenyekiti wa
Kamati namba mbili Shamsi Vuai Nahodha(katikati) na Mwanasheri Mkuu wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Othaman Masoud Othaman(kulia)
Wajumbe
wa Kamati namba mbili wakimsikiliza Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Pius Msekwa (hayupo pichani) wakati anatoa
ufafanuzi leo mjini Dodoma kuhusu hati ya Muungano baada ya wajumbe hao
kumuomba aende kuwaelimisha juu ya hati hiyo.Mwenyekiti
wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta(kulia) akizungumza na wajumbe
wa Kamati namba Sita (6) ya Bunge hilo leo mjini Dodoma wakati
akitembelea Kamati mbalimbali kujionea maendeleo ya uchambuzi wa vifungu
mbalimbali vya rasimu ya Katiba mpya kwa sura ya Kwanza na Sita.
Wengine ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Stephen Massato Wassira(katikati)
na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Maua Abeid Daftari (kushoto)
Picha na Bunge la Maalum la Katiba
EmoticonEmoticon