SHIRIKA LA POSTA TANZANIA LATOA TAARIFA JUU YA UTEKELEZAJI WAKE WA MPANGO KABAMBE WA MIAKA KUMI (2014-2023).
Pichani
ni Postamasta Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta
Tanzania,Bwa.Deos Mndeme akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye Makao
makuu ya Ofisi hizo jijini Dar mapema leo kuhusiana na taarifa juu ya
utekelezaji wa Mpango Kabambe wa miaka kumi (2014-2023) wa shirika la
Posta Tanzania,wakati Tanzania ikielekea kuadhimisha miaka 50 ya Muungano.
Pichani
Kulia ni Meneja Mkuu Uendeshaji wa Biashara,Bwa.Fortunatus Kapinga
akifafanua jambo kuhusiana na taarifa juu ya utekelezaji wa Mpango
Kabambe wa miaka kumi (2014-2023) wa shirika la Posta Tanzania,wakati
Tanzania ikielekea kuadhimisha miaka 50 ya Muungano.Amesema kuwa Shirika
la Posta limeanza utekelezaji mpango kabambe wa miaka kumi (2014-2023)
ikiwa ni dira na mwelekeo wa kuliongoza shirika hilo liweze kujiendesha
kibiashara,kubuni na kutoa huduma mbadala,kutumia teknolojia maridhawa
na kukidhi mahitaji ya soko la huduma za mawasiliano jumuishi.Kushoto
kwake ni Postamasta Mkuu na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Posta
Tanzania,Bwa.Deos Mndeme.
Pichani
kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masuala ya Kimataifa wa
Shirika la Posta Tanzania,Bwa.Elias Madule akifuatilia mkutano huo akiwa
sambamba na mdau mwingine wa shirika hilo la Posta.
Waandishi
wa Habari wakisikiliza taarifa juu ya utekelezaji wa Mpango Kabambe wa
miaka kumi (2014-2023) wa shirika la Posta Tanzania kutoka kwa Viongozi
wakuu wa Shirika hilo,katika mkutano uliofanyika mapema leo,ndani ya
Makao makuu ya Ofisi hizo jijini Dar.
EmoticonEmoticon