TUZO ZA MAKOCHA ZAJA MACHI 2014

January 09, 2014

Na Daud Julian, Morogoro 

TUZO ya makocha wa mpira wa miguu Tanzania ‘Tanzania Football Coaches Awards 2014’ inatarajiwa kutolewa mapema mwezi machi, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na TANGA RAHA BLOG, ofisa mtendaji wa tuzo hizo, Fredrick Luunga alisema lengo hasa ni kuthamini mchango wa makocha wazawa na wa kigeni katika kuendeleza mchezo wa soka hapa nchini.
Luunga alisema kwa miaka mingi, makocha wamekuwa wakifanya kazi hiyo katika mazingira magumu na wamekuwa hawathaminiwi vya kutosha kutokana na mchango wanaoutoa katika kupigania maendeleo ya mchezo huo.
Alisema, anaamini tuzo hiyo itakayokuwa ikitolewa kila mwaka, itasaidia kuibua ari mpya na kuwaongezea morali ya kufanya kazi makocha.
Kocha mkongwe, Alhaj Abdallah Athumani Seif 'King Kibaden' anashikilia tuzo ya kocha wa bora wa Ligi Kuu

“Hii tuzo kwa makocha wa mpira wa miguu ni ya kwanza kutolewa hapa nchini licha ya kuwepo kwa aina mbalimbali ya tuzo, nafikiri hii itakuwa chachu kwa makocha na wadau wengine”, alisema.
Luunga alizitaja baadhi ya tuzo hizo kuwa ni kocha bora wa mwaka, kocha wa makipa, kocha mkongwe mwenye mafanikio zaidi, kocha bora chipukizi, kocha bora wa kike, kocha bora wa kigeni, kocha wa kigeni aliyewahi kupata mafanikio makubwa alipokuwa akifundisha soka Tanzania na kocha bora mtanzania anayefundisha nje ya nchi.
Baadhi ya makocha wa soka wazawa ambao huenda wakapata tuzo hizo iwapo watachaguliwa ni Abdallah Kibaden, Jamhuri Kiwelu ‘Julio’, Charles Boniface Mkwasa, Fred Felix Minziro, Juma Mwambusi, John Simkoko, Mohamed Msomali, Ken Mwaisabula, Jumanne Chale, Meck Maxime, Seleman Matola, Adolf Rishard, Hemed Mumba, Joel Bendera, Athuman Bilal, John Tegete, Mlage Kabange na Henry Mkanwa.
Wengine ni Amri Said, Shadrack Nsajigwa, John Tamba, Charles Mwakambaya, Amri Ibrahimu, Patrick Mwangata, Juma Pondamali, Idd Pazi, Peter Manyika, Joseph Lazaro na Mohamed Kampira.
Baadhi ya makocha wa kigeni waliopo na waliowahi kufundisha nchini ni Zdravko Logarusic, Joseph Marius Omog, Yusuph Chipo, Jackson Mayanja, Kim Poulsen, Marcio Maximo, Ernie Brandts, Jack Chamangwana, Stewart Hall, Patrick Phir, Raoul Shungu, Popadic na Patrick Liewig.
 
CHANZO.BINZUBEIRYBLOG

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »