Na Oscar Assenga, Korogwe.
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Mkoa wa Tanga
(UVCCM),Abdi Makange amewataka makatibu umoja huo ngazi ya wilaya na kata kuachana
na makundi ya uchaguzi mwaka 2014-2015 kwani hali hiyo itawafanya kushindwa
kutimiza wajibu wao ipasavyo na kuleta mpasuko ndani ya umoja huo.
Kauli hiyo aliitoa wakati wa kikao cha baraza la Vijana
wilaya ya Korogwe ambacho kilihusisha wajumbe kutoka wilaya ya Korogwe mjini na
Vijijini ikiwa ni ziara ya siku ya pili ya Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mkoa wa
Tanga,Abdi Makange ya kukagua uhai wake na kusikiliza kero za wananchi maeneo
mbalimbali mkoani Tanga.
Makange alisema makundi hayana nafasi kwa wakati huu kwani
wao wamedhamiria kuhakikisha yanayaondoa kwa kutowafumbia macho viongozi wa
aina yoyote ambao watabainika kuanzisha makundi ndani yao.
Alisema wakati umefika kwa vijana kufanya uamuzi wa busara
na kujitenga na makundi hayo pamoja na kuachana na tabia ya kuwanyooshea vidole
watu kutokana na matendo yao bali hali hiyo itumike kwenye utendaji wao.
Aidha aliwataka
vijana kuacha kujiingiza katika makundi ya aina yoyote ile badala yake
wahakikishe wanakuwa mstari wa mbele kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali
kwenye chaguzi zijazo kwani wanahaki na wajibu wa kufanya hivyo lengo likiwa
kusukuma gurudumu la maendeleo ya wananchi na jamii nzima kwa ujumla.
“Vijana wakiingia
kwenye makundi ya uchaguzi muda huu naambieni mtapata dhambi kubwa sana ambayo haitafutika
maishani mwenu hivyo nawasihi kuachana na mawazo hayo “Alisema Makange
Hata hiyo Katibu huyo aliagiza kuandikiwa barua za kupewa
onyo makatibu vijana ngazi ya kata ambao walioshindwa kuhudhuria mkutano huo
pamoja na kuwataka kabla hawajafanya hivyo wao wenyewe waandike barua za
kujieleza.
Makange aliwataka makatibu hao kutafuta vyanzo vya
kuwaingizia mapato katika maeneo yao
kwa kubuni miradi ya kuendeleza kata zao ili kuepukana na suala la kuwa omba
omba.
Katika ziara hiyo ilihitimishwa na Mwenyekiti huyo
kutembelea ujenzi wa shule ya sekondari Kwagunda ambapo walihaidi kuchangia
mifuko 10 ya saruji ili kuharakisha ujenzi huo ambao utakapokamilika utawasadia
wanafunzi katika mazingira mazuri.
EmoticonEmoticon