RC GALLAWA AKABIDHI ZAWADI ZA KRISMAS NA MWAKA MPYA ZILIZOTOKA KWA JK KWA MAKAZI YA WAZEE WASIOJIWEZA MISUFINI MUHEZA.

December 24, 2013

                                    
 
Na Mbaruku Yusuph,Muheza.
 IMEWEKWA DESEMBA 24 SAA 3:26 MCHANA.
 MKUU wa Mkoa wa Tanga, Luteni Mstaafu Chiku Gallawa leo amekabidhi zawadi za sikukuu ya Krismas na mwaka mpya kutoka kwa Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanga Dkt Jakaya Mrisho Kikwete katika eneo la makazi ya wazee wasiojiweza la Misufini kata ya Ngomeni wilayani Muheza

Zawadi zilizokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa Gallawa ni mchele kilo 150,mbuzi watatu(3) na Mafuta ya Chakula lita 40,michezo ya sabuni pamoja na katoni moja y chumivi vyote vikiwa na thamani ya sh.615,000.


Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hizo, Gallawa ametoa wito kwa kila mwananchi kuweka utaratibu wa kusaidia wale wote ambao hawana uwezo na wenye shinda hasa katika kipindi hiki cha sikukuu ya krismas na mwaka mpya kama alivyofanya Mh.Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Aidha amewataka wananchi kushehereka sikukuu ya krismas na mwaka mpya kwa amani na utulivu kwa kuweka msisitizo kuwa wajiepueshe na vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani.

Mkuu huyo wa mkoa amewataka wananchi kutoa taarifa kwa vyombo vya husika pindi wanapoona katika maeneo yao kuna viashiria vya uvunjifu wa amani ikiwemo kuliweka jiji la Tanga katika hali ya usafi .

Wakati huo huo, Mkuu huyo wa mkoa ameaswa kuacha kuendesha magari mwendo kasi hasa katika kipindi cha sikukuu ya krismas na mwaka mpya kutokana na kuwa wananchi wengi hutumia vyombo vya usafiri kwenda mapumzikoni .

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »