Mkuu
wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone akizungumza kwenye mkutano wa wadau
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)
uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Katala Beach hoteli mjini
Singida.
Mjumbe
wa bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Lyidia Choma (kulia)
akitoa taarifa yake kwenye siku ya wadau wa Mfuko huo na ule wa Afya ya
Jamii (CHF).Mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Katala
Beach Hotel mjini Singida. Kushoto (aliyeshika mike) ni Meneja wa NHIF
mkoa wa Singida, Agnes Chaki.
Mkurugenzi
wa takwimu na uhai wa mfuko wa NHIF makao makuu, Michael Mhando akitoa
nasaha zake kwenye mkutano wa wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na
Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa
Katala Beach Hotel mjini Singida. Kushoto ni mkuu wa mkoa wa
Singida,Dk.Parseko Kone, Wa kwanza kulia ni kaimu Mganga Mkuu wa mkoa wa
Singida,Dk.Mussa Kamala, Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi na
katibu tawala mkoa wa Singida,Liana Hassan.
Mkuu
wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, (wa pili kulia) akifuatilia kwa
makini mada zilizokuwa zikitolewa kwenye mkutano wa siku ya wadau wa
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii. Wa kwanza
kulia ni Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bi. Lyidia
Choma.Wa tatu kulia ni Katibu Tawala mkoa wa Singida, Liana Hassan
na,Mkuu wa Wilaya ya Singida,Queen Mlozi na kaimu Mganga Mkuu mkoa wa
Singida,Dk.Mussa Kimala.
Na Nathaniel Limu
Zaidi
ya asilimia 73 ya kaya za mkoa wa Singida, hazijajiunga na mfuko wa
afya ya jamii (CHF), hali inayochangia wanafamilia watibiwe bila
utaratibu maalum.
Hayo
yamesemwa na mkuu wa moa wa Singida, Dk. Parseko Kone, wakati
akizungumza kwenye uzinduzi wa mkutano wa siku ya wadau wa Mfuko wa
Taifa Bima ya Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii (NHIF) wa mkoa wa SIngida.
Akifafanua,
amesema kati ya kaya 259,251 za mkoa wa Singida, ni kaya 45,575 tu,
ndizo zilizojiunga na mfuko wa afya ya jamii kati ya mwaka 1998 na
Septemba 30 mwaka huu. Hii ni sawa na asilimia 17.6 tu.
“Hata
hivyo,wilaya ya Iramba imekuwa ikifanya vizuri katika uandikishaji wa
wananchi, kwani takwimu zinaonyesha hadi Septemba 30 mwaka huu,
wamekwisha andikisha asilimia 50.3 ya kaya zilizolengwa. Hali hii
inaonyesha kuwa viongozi bado hatujatimiza wajibu wetu wa kuhamasisha
wananchi kujiunga na mfuko huu”, amesema Dk.Kone.
Aidha,
mkuu huyo wa mkoa, amesema pia inawezekana watoa huduma wamekuwa ni
chanzo cha kuwakatisha tama wananchi waliojiunga na hivyo, kuwafanya
wananchi wengine wasite kujiunga na Mfuko huu.
“Kwa
kuwa wadau wote tumekutana hapa leo, ni nafasi yetu kuangalia nini
sababu ya kuzorota kwa utaratibu huu ambao katika baadhi ya halmashauri
hapa nchini, umeimarika zaidi",amesema Dk.Kone.
Awali
mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),
Lyidia Choma, alisema Mfuko huo umeidhinisha shilingi bilioni 10, ili
zitolewe kwa watoa huduma kuwawezesha kupata vifaa tiba na kukarabati
maeneo yao ya kutolea huduma.
“Utaratibu
huu ni mikopo ya bei nafuu ambayo hairejeshwi kwa fedha taslimu,
isipokuwa kwa kukatwa katika madai ambayo mtoa huduma anawasilisha kwa
Mfuko”,amefafanua.
Alifafanua
kuwa kwa mkopo wa vifaa tiba, mkopo hurudishwa kwa makato ya asilimia
10 ambayo hulipwa ndani ya miezi 24 na mikopo ya ukarabati wa maeneo ya
kutolea huduma, ni miezi 36.
Kauli mbiu ya mwaka huu, ni Afya Bora kwa wote sasa kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
EmoticonEmoticon