Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
TANZANIA imeongoza katika orodha ya tatu ya matajiri wapya wakubwa Afrika iliyotolewa na jarida la Forbes, mfanyabishara Rostam Aziz aliyeacha siasa kwa shinikizo la chama chake, CCM ili kubaki kwenye biashara pekee akitajwa kuwa tajiri zaidi nchini.
Rostam aliyejiuzulu Ubunge wa Igunga mwaka 2011, jarida la Forbes limesema ana utajiri wa thamani ya dola za Kimarekani Bilioni 1.![]() |
| Mtanzania tajiri zaidi; Rostam Aziz ana zaidi ya dola Bilioni 1 |
Rasilimali
zake kubwa ni pamoja asilimia 35 ya hisa katika kampuni ya Vodacom
Tanzania, kampuni kubwa ya simu za mkononi Tanzania, ikiwa na wateja
zaidi ya milioni 9.5; kampuni ya madini ya Caspian Mining, pamoja na
biashara anazofanya kwa kushirikiana na na bilionea wa Hong Kong, Li
Ka-shing. Azizi pia amewekeza Dubai na Oman.
Mtanzania
mwingine, Reginald Mengi ni tajiri mkubwa wa pili Afrika katika
uwekezaji kwenye sekta ya Habari, baada ya Koos Bekker wa Afrika Kusini.
Binafsi, Mengi anamiliki kampuni ya IPP yenye magazeti 11, Televisheni
tatu na vituo 10 vya Redio.
Rasilimali
nyingine za Mengi ni migodi ya dhahabu, kampuni kadha za madini na
kampuni ya soda ya Coca-Cola. Ana utajiri wa jumla ya dola za Kimarekani
Milioni 550 kwa mujibu wa tathmini za FORBES.
Mtu
mpya katika orodha ya matajiri 50 wa Forbes 50 ni Mualgeria, Issad
Rebrab, ambaye ameingia na tajiri wa thamani ya dola Milioni 3.2. Rebrab
ni muanzilishi wa Cevital, kampuni ya familia inayotengeneza sukari,
mafuta ya kupikia na jibini. Cevital pia inamiliki viwanda vya
uzalishaji bidhaa za kusambaza.
Bilionea
wa Kenya na Afrika Mashariki, Vimal Shah ameingia kwenye orodha hiyo na
utajiri wake wa dola Bilioni 1.6. Shah, baba yake na kaka yake kwa
pamoja wanamiliki kampuni ya mafuta ya kupikia Bidco.
Pato
la mwaka la kampuni hiyo ni dola Mlioni 500. Bidco pia inatengeneza
unga wa chakula na sabuni za manukato katika nchi 14 Afrika. Pia ni
muwekezaji wa Tatu City, kampuni mpya yenye thamani ya dola Bilioni 3
ya Satellite itakayokuwa na maskani yake, Nairobi.
Mmorocco,
Aziz Akhannouch ana utajiri wa dola Bilioni 1.4 kutokana na kumiliki
kwake kampuni ya Akwa Group, iliyoanzishwa na baba yake ambayo kwa sasa
inamiliki kampuni za Afriquia Gas na Maghreb Oxygene pamoja na vyombo
vya habari, uwekezaji wa ardhi na hoteli. Akhannouch kwa sasa ni Waziri
wa Kilimo na Uvuvi wa Morocco. Mkewe, Salwa Idrissi, anamiliki majengo
ya kifahari.
Aspen
Pharmacare, walioshiriki kuanzisha Gus Attridge ya Afrika Kusini
wameingia kwenye orodha hiyo kwa utajiri wao wa dola Milioni 525.
Mtanzania,
Mohammed ‘Mo’ Dewji anaingia katika orodha hiyo kwa utajiri wake wenye
thamani ya dola milioni 500. Ni Mtendaji Mkuu wa kampuni ya METL,
iliyoasisiwa na baba yake, Gulam Dewji.
Baada ya kumaliza masomo ya
biashara katika chuo Kikuu cha Georgetown, Marekani alirejea nyumbani
kuendeleza biashara za baba yake na pia kwa sasa ni mwanasiasa, Mbunge
wa jimbo la Singida Mjini.

EmoticonEmoticon