NA BONIFACE WAMBURA,DAR ES SALAAM.
Maombi
ya vitambulisho kwa waandishi wa habari (Accreditation) wanaotaka
kuripoti Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil
kwa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) yataanza
kupokelewa kwa mtandao Desemba 7 mwaka huu kupitia akaunti ya FIFA Media
Channel.
Mwisho
wa kupokea maombi hayo itakuwa Januari 31 mwakani, hivyo kwa waandishi
wanaotaka kupata vitambulisho hivyo ni lazima wawe na akaunti ya FIFA
Media Channel pamoja na utambulisho wa mtumiaji wa akaunti hiyo (user
ID).
Kwa
mujibu wa FIFA, kila nchi itapewa idadi maalumu ya nafasi kwa waandishi
(waandishi wa kawaida pamoja na wapiga picha) baada ya mechi za mchujo
za Kombe la Dunia kumalizika ambapo vigezo mbalimbali vitazingatiwa
ikiwemo nchi kufuzu kwa fainali hizo.
Hivyo,
nchi ambayo itakuwa imefuzu itakuwa na nafasi zaidi kulinganisha na
zile ambazo hazitakuwa na timu katika fainali hizo za Brazil.
Mgawanyo
wa nafasi zitakazotolewa kwa Tanzania utapangwa na Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa
Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kulingana na maombi yatakayokuwa
yamewasilishwa FIFA kupitia FIFA Media Channel.
TFF
inatoa mwito kwa waandishi wa habari za mpira wa miguu ambao hawana
akaunti FIFA Media Channel kuhakikisha wanakuwa nayo mapema ili waweze
kutuma maombi yao.
EmoticonEmoticon