Na Oscar Assenga, Tanga.
NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto ,Ummy
Mwalimu amesema serikali inatambua na kuthamini ushiriki wa wanawake katika
shughulia mbalimbali za maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Mwalimu alitoa kauli hiyo leo wakati akifungua mafunzo ya
wasichana waelimishaji rika mkoa wa Tanga yaliyohusisha wasichana wapatao 150
kutoka wilaya za Muheza,Lushoto, Pangani,Mkinga na Tanga yenye lengo la
kuwajengea uwezo na kuratibiwa na shirika lisilo la kiserikali la maendeleo ya wanawake (TAWODE).
Alisema hali hiyo inajidhihirisha katika malengo ya
millennia,Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ikiwa ni mkakati wa pili wa kukuza
uchumi na kuondoa umaskini (Mkukuta 11) na Sera ya Taifa ya wanawake na Jinsia
ya mwaka 2000.
Naibu Waziri huyo alisema wizara yake inajukumu kubwa la
kuwajengea uwezo wanawake na wanaume ili waweze kushiriki katika ngazi zote za
utekelezaji wa miradi na mipango mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kufaidika sawa
kwenye maendeleo yao.
Aidha alisema jambo jengine ni kuhamasisha na kuwezesha
jamii kuwapatia watoto haki ya kuishi,kuendelezwa, kulindwa,kutokubaguliwa na
kushiriki katika maendeleo ya Taifa na hivyo itatoa miongozo ya kuzuia na
kupinga aina zote za ukatili na ubaguzi wa kijinsia kwa wanawake na watoto.
“Ni ukweli
usiopingika kuwa ukimwendeleza mwanamke, umeendeleza Taifa zima na kuwekeza kwa
mwanamke ni kuwekeza katika taifa endelevu “Alisema Mwalimu
Alitoa wito kwa wadau wote kuchukua hatua za kumuwezesha
mtoto wa kike na kushughulikia mazingira hatarishi yanayomkabili katika kipindi
cha ukuaji ili wasipate mimba za utotoni ikiwemo maambukizo ya virusi vya
ukimwi na kukosa au kupunguza fursa zake mbalimbali za kujiendeleza.
Awali akuzungumza katika mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa
TAWODE ,Fatuma Hamza Mganga alisema madhumuni ya semina hiyo ni kuwajengea uwezo wasichana wenye umri
kati ya miaka 10 mpaka 24 na kuchochea uwezo na ubora wa kutambua ueledi na
umuhimu wao katika maendeleo yao na jamii kwa ujumla.
Mganga alisema pia semina hiyo ilikuwa na madhumuni ya
kuwawezesha katika kujiamini, kujitambua na kuthubuti.
Mwisho.
EmoticonEmoticon