NA OSCAR ASSENGA,PONGWE.
KITUO cha Afya Kata ya
Pongwe katika Halmashauri ya Jiji la Tanga kinakabiliwa na changamoto
mbalimbali hali ambayo inapelekea kushindwa kufikia malengo yao waliojiwekea hasa katika utoaji huduma
kwa wagonjwa wanaofika kituoni hapo.
Mganga Mfawidhi wa Kituo
hicho,Ally Bughe alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na Tanga Raha ofisini kwake na kueleza kuwa licha ya kuwepo hali hiyo lakini pia kituo hicho
hakina uzio kitendo ambacho kinapelekea mifugo kuingia mpaka kituo wakati wa
utoaji wa huduma.
Bughe alisema kituo hicho
pia kinawakabili ni kukosekana kwa maabara ya kisasa kwa ajili ya kuchukulia
vipimo vya wagonjwa licha ya kuwa na wataalamu wa kutosha.
Alisema licha ya kuwepo
changamoto hizo wanatarajia kuanza kufanya upasuaji lakini hawana wodi maalumu
ya kuwalaza wagonjwa watakaofanyiwa upasuaji huo.
Aliongeza kwa kusema kuwa
kituo hicho hakina gari maalumu la kubebea wagonjwa pindi wanapozidiwa na
kuhitajika kupelekwa katika hospitali ya mkoa Bombo zaidi ya usafiri wa pick up
ambayo sio salama kwao.
Aidha wanaiomba
halmashauri ya Jiji la Tanga kuangalia namna ya kukabiliana na changamoto hizo
ili kuweza kuzipatia ufumbuzi pamoja na kuhakikisha wanaondoa matatizo hayo.
Mwisho.
EmoticonEmoticon