NA OSCAR ASSENGA,TANGA
TIMU ya Mbeya City ya Mbeya leo imefanikiwa kuifunga
Mgambo Shooting ya Tanga bao 1-0 ikiwa ni mechi ya Ligi kuu Tanzania bara
uliopigwa kwenye dimba la soka Mkwakwani.
Mchezo huo ulikuwa mkali na wenye upinzani mkali
ambapo Mbeya City waliandika bao lao la kwanza katika dakika ya 20 kupitia
Jeremia John baada ya kumalizia kazi nzuri iliyokuwa imefanywa na Alex Seth.
Bao hilo lilidumu mpaka timu zote zinakwenda
mapumziko ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi ya mashambulizi kwa timu
zote kushambuliana kwa zamu baada kufanya mabadiliko kwenye baadhi ya wachezaji
wao.
Mabadiliko kwa upande wa Mbeya City waliwatoa Alex Seth,Jeremia
John na Deus Kaseke ambao nafasi zao zilichukuliwa na Hamad Kibopile,Fransis
Casto na Peter Mapunda.
Kwa upande wa Mgambo Shooting wao waliwatoa Mohamed
Samata na kuingia Twaha Mihinga kutokana na mabadiliko hayo mgambo waliweza kufanikiwa
kucheza kwa vema huku walilishambulia lango la wapinzani wao bila mafanikio
yoyote.
Katika dakika ya 72 mgambo shooting walipata pigo
baada ya mchezaji wao Salum Mlima kuonyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi wa mchezo
huo,Oden Mbaga kutoka DSM kwa kumchezea rafu mchezaji wa Mbeya City Yusuph
Wilson.
Kikosi cha Mbeya City leo ni Gk,David Burhan,John
Kabanda,Hassan Mwasapili,Yusuph Abdallah,Deogratius Julius,Anthony
Matogolo,Alex Seth,Steven Mazanda,Paul Nonga,Jeremia John na Deus Kaseke.
Mgambo Shooting waliwakilishwa na Gk
JohnKavishe,Salum Mlima,Ramadhan Kambwili,Salum Kipanga,Bakari Mtama,Novart
Lufunga,Nassoro Gumbo,Mohamed Samata,Mohamed Netto,Malimi Busungu na Peter
Mwalyanzi.
EmoticonEmoticon