WANAWAKE WATAKIWA KUTOKA TAARIFA ZA UNYANYASAJI KWA JESHI LA POLISI DAWATI LA JINSIA

September 29, 2013
NA ELIZABERTH KILINDI,TANGA.
WANAWAKE mkoani hapa  wametakiwa kutoa taarifa kwa  jeshi la polisi dawati la unyanyasaji kuhusiana na vitendo hivyo vinavyoendelea katika jamii zao.

Naibu Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu, alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki kwa niaba ya Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda katika uzinduzi wa mtandao wa kupinga ukatili wa kijinsia.

Naibu waziri huyo alisema kuwa nchi yetu inakabiliwa na changamoto kubwa ya vitendo hivyo vya kikatili na hivyo kutotolewa taarifa sehemu husika.

Aidha alisema kuwa asilimia 39 ya wanawake kati ya tisa, sita wamekuwa  wakifanyiwa ukatili wa kijinsia lakini wamekuwa na woga wa kutoa taarifa katika madawati ya jeshi la polisi ili kuweza kusaidiwa kwa namna moja au nyingine.

“Tatizo wanawake wamekua awatoi  taarifa za unyanyasaji sehemu husika ilikuweza kusaidi wa hivyo basi inapelekea vitendo hivi kuendelea  kuiangamiza jamii"alisema Naibu Waziri Ummy

Alisema pia kuna baadhi  ya watuhumiwa wa vitendo vya unyanyasaji kwa watoto wa kike kutumia nguvu ya fedha kurubuni familia ili wasifike mahakamani kutoa ushaidi wa kesi hizo.

Sambamba na hayo alisema kuwa kupinga unyanyasaji wa kijinsia ni vema kama  watawashirikisha pia na wanaume kwa kuwapa elimu hiyo ya unyanyasaji. 

Kwa upande wa mkurugenzi Mtendaji  wa taasisi isiyo ya kiserikali Tree Of Hope Fortunata Manyereza alisema kuwa lengo la kuzindua mtandao  huo ni kupunguza ukatili wa kuijinsia unaondelea katika jamii zetu.

Manyereza alisema wamesaidia wanawake  wengi kupitia msaada wa kisheria ambapo kesi 30 zipo mahakamani na tisa wameshinda hivyo tunahakikisha ushirikiano katika suala hilo unyanyasaji.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »