BAO la dakika ya 87 ambalo lililofungwa na Yayo Lutimba limeipa ushindi Coastal Union kwenye mechi yao ya Kirafiki na Mafunzo ya Zanzibar mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.
Lutimba ambaye alisajiliwa na Coastal Union akitokea URA ya Uganda na aliyeingia kipindi cha pili aliweza kutumia vema pasi ya Mohamed Banka na kuweza kufanikisha kufunga bao hilo ambalo liliwafanya mashabiki wa soka mkoani hapa kulipuka kwa shangwe.
WACHEZAJI WA MAFUNZO NA COASTAL UNION WAKISALIMIANA KABLA YA KUANZA MCHEZO HUO AMBAPO COASTAL UNION WALIWEZA KUIBUKA NA USHINDI WA BAO 1-0. |
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo kila timu iliweza kuingia uwanjani hapo ikiwa na hari kwa timu zote kufanya mabadiliko kwa Coastal Union kuwatoa Othumani Tamim,Mbwana Bakari,Danny Lyanga,Soud Mohamed, na Atupele Green.
KOCHA MKUU WA COASTAL UNION YA TANGA,HEMED MORROCO KULIA MWENYE TISHTI NYEKUNDU AKITETA JAMBO NA KOCHA WA MAFUNZO YA ZANZIBAR,MOHAMED KACHUMBARI KABLA YA MECHI YAO KUANZA LEO. |
Ambao nafasi zao zilichukuliwa na Masumbuko Keneth,Mohamed Banka,Yayo Lutimba,Marcus Ndehele na Abdi Banda ambao walichukua chachu kwa kuleta ushindi kwenye kikosi cha Mafunzo na kuipa ushindi timu yao kutokana na kucheza vema.
WACHEZAJI WA MAFUNZO WAKIPASHA KWENYE UWANJA WA MKWAKWANI KABLA YA KUANZA MECHI YAO NA COASTAL UNION YA TANGA LEO |
Coastal Union iliwakilishwa na Gk Said Lubawa,Mbwana Bakari,Othuman Tamim,Philipo Mugenzi,Yusuph Chuma,Razack Khalfan,Danny Lyanga,Soud Mohamed,Atupile Green,Pius Kisambale na Abdallah Othuman.
Huku Mafunzo ikiwakilishwa na Gk Abdallah Swamadu,Abdul Halim,Haji Abdi,Yusuph Makame,Said Mussa,Hassan Ahmada,Hamad Haji,Haji Mwambe,Sadick Habibu,Mohamed Ally na Walid Ibrahim.
EmoticonEmoticon