NA BONIFACE WAMBURA,DAR ES SALAAM.
Timu
za Kimondo SC ya Mbeya na Kurugenzi ya Mafinga zitatumia viwanja vya
Mbozi na Mafinga kwa ajili ya mechi za Ligi Daraja la Kwanza (FDL)
inayoanza Jumamosi (Septemba 14 mwaka huu).
Kimondo
SC sasa itatumia Uwanja wa CCM Vwava ulioko wilayani Mbozi badala ya
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine wa jijini Mbeya. Nayo Kurugenzi itatumia
Uwanja wa Wambi ulioko Mafinga mkoani Iringa badala ya Uwanja wa
Makambako ulioko mkoani Njombe.
Mechi
za fungua dimba FDL msimu huu zitakuwa kati ya Burkina Faso na Polisi
Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro, Mkamba Rangers na
Lipuli ya Iringa kwenye Uwanja wa CCM Mkamba, Majimaji na Mlale JKT
kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea na Kimondo na Kurugenzi kwenye
Uwanja wa CCM Vwawa katika mechi za kundi B.
Septemba
14 mwaka huu Tessema na Green Warriors zitaoneshana kazi Uwanja wa
Karume, Dar es Salaam. Siku inayofuata (Septemba 15 mwaka huu) Transit
Camp na Polisi Dar (Mabatini mjini Mlandizi) wakati mechi nyingine za
kundi hilo la A zitakuwa kati ya Villa Squad na African Lyon (Karume) na
Ndanda FC na Friends Rangers (Nangwanda Sijaona, Mtwara).
Kundi
C ni Polisi Mara na Polisi Dodoma (Uwanja wa Karume, Musoma), Kanembwa
JKT na Polisi Tabora (Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma), Stand United
na Mwadui (Kambarage, Shinyanga) wakati Pamba na Toto Africans
zitamenyana Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
EmoticonEmoticon