NA BONIFACE WAMBURA,DAR ES SALAAM.
Temeke
imejiweka katika nafasi nzuri ya kucheza robo fainali ya michuano ya
Copa Coca-Cola kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 baada ya leo
(Septemba 10 mwaka huu) asubuhi kuizamisha Rukwa mabao 5-1.
Hadi
mapumziko katika mechi hiyo ya kundi B hatua ya Fainali za Taifa
iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam,
washindi walikuwa mbele kwa mabao 3-0.
Mabao
ya washindi yalitiwa wavuni na Constantine Katepa aliyefunga dakika ya
28, Patrick Ambrose dakika ya 36 huku Hamisi Kajole akipiga mawili
dakika ya 43 na 71. Bao la nne lilifungwa dakika ya 46 na Ramadhan Juma.
Rukwa
ambayo kwa matokeo hayo imeshatolewa ilipata bao lake dakika ya 51
kupitia kwa Francisco Nkanga. Timu nyingine katika kundi hilo ni Geita
na Ilala.
Robo
Fainali ya michuano hiyo itaanza keshokutwa (Septemba 12 mwaka huu).
Kila kundi linatoa timu mbili kucheza hatua hiyo katika mashindano hayo
yanayodhaminiwa na kampuni ya Coca-Cola.
EmoticonEmoticon