TIMU ya African Sports "Wanakimanumanu"wanatarajiwa kuwa na mkutano na wanachama wao kesho saa kumi na moja jioni makao makuu ya klabu hiyo barabara 12 jijini Tanga lengo likiwa ni kujadili maendeleo ya timu hiyo.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Klabu hiyo,Said Karsandas alisema kwenye kikao hicho kutakuwa na agenda
mbalimbali ambazo zitajadiliwa kwa ajili ya mustakabali wa timu hiyo kongwe hapa nchini.
Karsandas alisema licha ya kuzungumzia maendeleo lakini pia watatumia muda huo kujadili suala la uchaguzi mkuu wa timu hiyo ambao utafanyika katikati ya mwezi huu .
Alisema wanachama pekee ndio ambao wataruhusiwa kushiriki katika mkutano huo ambao ni muhimu sana kwa ajili ya maendeleo yao pamoja na kupanga mikakati ya ushiriki wao kwenye ligi ya mkoa msimu huu.
EmoticonEmoticon