PONDAMALI :MZIKI UNALIPA ZAIDI KULIKO MPIRA.

August 11, 2013

Na Oscar Assenga,Tanga.
MSANII Mpya wa Muziki wa BongoFleva hapa nchini,Juma Pondamali “Mensa”amesema mziki huo unalipa sana kuliko hapa mchezo wa mpira wa miguu ila itatagemea na umahiri ulionao katika kutoa mashairi mazuri.

Akizungumza na Tanga Raha,Pondamali ambaye hivi sasa anatamba na wimbo wake “Pesa baba yako nani”ambao ameirekodi kwenye studio za Suleshi alisema ameamua kuingia kwenye mziki huo sio kwa kutania bali ni dhamiri yake aliyekuwa nayo muda mrefu.

Pondamali alienda mbali zaidi na kueleza anamshukuru mwenyezi mungu kwa kumjalia kipaji cha utunzi mzuri na uimbaji kitu ambacho kitampa wakati mzuri wakati akiwa katika harakati zake za kuachia album lakini akisema wakati huu amepanga kuachia single tu.
    
“Ninamshukuru mwenyezi mungu amenijali kipaji kizuri cha utunzi na sio kama ninatania nimedhamiri kweli kufanya mziki kwa sababu unalipa kuliko ilivyo soka na unaweza kuuza single moja tu ukapata fedha nzuri “Alisema Mensa.

Aidha aliongeza kuwa licha ya kuimba mziki hatoweza kuiacha kazi yake aliyokuwa nayo hivi sasa kwani anaiheshimu na kuithamini hivyo atafanya mziki na kufundisha soka kwani kila kitu hapo kinawakati wake na muda.

Pondamali ambaye pia ni Kocha wa Makipa kwenye timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars”na timu ya Coastal Union ya Tanga alisema malengo yake makubwa ni kuhakisha anafanya vizuri kwa kutoa nyimbo mzuri ambazo zitaweza kumpa mafanikio zaidi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »