LIGI YA WILAYA YA KOROGWE KUTIMUA VUMBI OCTOBA 10 MWAKA HUU.

August 11, 2013
(Katibu wa Chama cha Soka wilaya ya Korogwe Zaina Kassama wa Tatu anayemfuatia Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa)

Na Safari Chuwa,Korogwe.
LIGI ya soka wilaya ya Korogwe inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Octoba 10 mwaka huu ambapo itachezwa katika viwanja ambavyo vitatangazwa baadae na chama cha soka wilaya ya Korogwe (KDFA).

Katibu wa Chama hicho,Zaina Hassani alisema maandalizi ya ligi hiyo yanaendelea vizuri na kueleza mpaka wakati huu timu nane zimejitokeza kuchukua fomu za kushiriki huku timu zaidi ya ishirikini zikitarajiwa kushiriki.

Hassani alizitaja timu ambazo zimechukua fomu ni Kilole,New Cap,Ngombezi,Nyota SC, Kwamndolwa, Liver Pool,Mombo Shooting na Millan FC na kutoa wito kwa timu nyengine kujitokeza kushiriki mashindano hayo.

Alisema ligi hiyo itachezwa kwenye vituo mbalimbali wilayani humo ambapo washindi kila kituo watakutana kwenye kituo kimoja ili kuweza kumpata bingwa wa wilaya hiyo.

Katibu huyo alisema baada ya kupatikana bingwa wa wilaya hiyo atapata fuksa ya kuungana na mabingwa wengine kutokana wilaya mbalimbali kucheza ligi ya mkoa.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »