Na Mwandishi Wetu, Tanga.
RAIS wa Miss Utalii nchini, Gidion Chipungahelo amesema
kampuni ya Kokoliko Disgner ndio kampuni pekee waliyoamua kuipa kibali cha kuwavalisha
washiriki wa Miss Utalii hapa nchini na nje ya nchi lengo likiwa ni kutambua
mchango wao kwenye tasnia hiyo.
Akizungumza jana, Chipungahelo alisema licha ya kuwavalisha
na kuwabuni mavazi washiriki wa miss Utalii hapa nchini lakini watawatangaza
kitaifa na kimataifa kwenye mashindano ya Tourist Model of the world
itakayofanyika mwezi septemba mwaka huu nchini Japan kwa kuwa nao.
Chipungahelo alisema suala lengine ambalo kampuni hiyo
itakalolifanya ni kuondoka nao hapa nchini kwenda kushuhudia shindano la Miss
Utalii Dunia ambalo litafanyika Equatorial Guinner desemba 10 mwaka huu.
“Mchango wa kampuni hiyo ni mkubwa sana hasa kwenye suala
zima la ubinunifu wa mavazi hivyo hii itakuwa fuksa adimu kwao kuwaonyesha
mavazi yao na mitindo mbalimbali kwenye nchi hizo “Alisema Chipungahelo.
Alisema safari nyegine ya tatu ambao watakuwa nao ni kwenye
shindano la Miss tournament Umoja wa Mataifa ambalo litafanyika Florida nchini
Marekani na kueleza watashirikiana na kampuni ya Sophia production ,kokoliko
kwa ajili ya kwenda kuwatangaza kama
wabunifu wa mavazi wa kitanzania.
Aliongeza kwa kuishukuru Kokoliko disgner kwa kushirikiana na
kampuni ya Sophia Production kwa kubuni na kutengeneza mavazi yaliyopelekea
kuchangia warembo walioshiriki mashindano hayo kutoka hapa nchini kufanya
vizuri.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Kokoliko Disgner,
Aisha Kisoki “Mama Sophia”alisema kampuni hiyo itaendelea kuwabunia mavazi
washiriki hapa nchini lengo likiwa ni kutangaza asili ya watanzania.
Mwisho.
EmoticonEmoticon