SERIKALI YA MTAA MUUNGANO YAONESHA MUELEKEO CHANYA KWENYE MAENDELEO

February 10, 2025
Na Mariam Mohamed Amry

MWENYEKITI wa Mtaa wa Muungano kata ya Goba Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, mkoani Dar es Salaam, Isack Maduhu amelezea mikakari mipya ya utendaji na hatua zilizochukuliwa katika sekta mbalimbali za kijamii ndani ya Mtaa wake ikiwepo Afya , Elimu , Miundombinu ya Maji na kadhalika.

Akizungumza na wananchi Februari 9, 2025 kwenye mtaa wake, Maduhu amesema kutakuwa na ujenzi wa Zahanati ya Mtaa wa Muungano ambayo itarahisisha ufanisi wa huduma ya Afya kwa wananchi.

Amesema kutatolewa vyandarua vyenye dawa kwa watoto chini ya Mwaka Mmoja na wajawazito kwa hati punguzo ili kudhibiti ugonjwa wa Malaria.

Aidha amesisitiza kuwa Serikali ya Mtaa inayotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitahakikisha kinajenga jamii yenye Afya bora, katika kipindi cha mwaka 2024 - 2029.

Katika Sekta ya Elimu ameunda utaratinu wa ziara wa kutembelea shule za awali, Msingi na Sekondari kuangalia majengo na maziingira yake.

Pamoja na hayo Maduhu amewahakikishia wananchi wa Mtaa wa Muungano kufanyika kwa ujenzi na upanuzi wa Miundombinu ya maji ili waweze kupata maji safi na salama .

"Mpaka sasa wananchi wameishaanza kuchukua fomu kwa ajiri ya kuonganishiwa huduma ya maji na na tayari mabomba yameshakabidhiwa katika shina namba nne na shina namba tano". Amesema Maduhu

Kwa upande wake Mwakilishi wa TARURA, Mkandarasi Cavine Lugendo amesema wamechukua hatua ya kuomba fedha ili kudhibiti athali za mvua zilizotokea mwaka jana na hadi mwaka huu mwanzoni na kuharibu Miundombinu ya barabara na Madaraja.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »