SHIRIKA LA UWASHEMU LAWAJENGEA UWEZO WAVUVI NA WAKULIMA WA MWANA WILAYANI MKINGA

February 10, 2025


Na Oscar Assenga, MKINGA.

SHIRIKA la Umoja wa Wasaidizi wa Msaada wa Kisheria wilayani Mkinga (Uwashemu) wamefanya warsha ya pamoja kati ya wakulima wa mwani na wavuvi wakiwemo wadau wengine ili kuwajengea uwezo wa kuhakikisha shughuli zao zinafanyika kwa amani katika maeneo yao.

Akizungumza wakati wa warsha hiyo kupitia mradi wa Kujenga Amani pamoja, Afisa wa Shirika hilo, Makange Omari Machemba ambapo alisema hiyo ni kuhakikisha wanafuata taratibu zilizopo ili kila mmoja aweza kushiriki vema katika shughuli zao za kujiingizia kipato kwa amani.

Alisema kwamba shirika hilo linafanya kazi kwenye mambo ya kutoa elimu ya sheria na kwa sasa wana miradi miwili ya kwanza upatikanaji haki Tanzania wanafadhiliwa na Shirika la LSF Dar na mradi huo umeishia mwezi wa Octoba mwaka jana na wana mradi wa kujenga amani pamoja wanafadhiliwa na Shirika la 4h Tanzania wanapata ufadhili kutoka We World .

Alisema mradi huo wanaufanya kwenye kata za Moa na Boma ambapo mradi unahusisha wakulima wa mwani na wavuvi huku akieleza kwamba utakuwa na manufaa makubwa kusaidia kuondosha changamoto zilizopo

Awali akizungumza wakati akifungua Warsha ya Mradi wa Kujenga Amani, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wilaya ya Mkinga Elizabert Malali alisema kwamba njia ya midahalo ni salama katika kutatua changamoto na kuzuia migogoro na kujenga amani katika maeneo mbalimbali

Alisema kwamba anaamini kupitia kikao hicho watapata wasaa mzuri wa kujadiliana kwa kina na uzoefu wao wauwasilishe uwasaidie wao kama watendaji wa serikali waone kwenye meneo yapi ya kuongeza nguvu ili kwa pamoja waweze kuwa na jami yenye utulivu inaweza kuzalisha na kujiletea maendeleo yake.

“Wilaya yetu ya Mkinga ni tajiri kwa sababu Mungu ametujalia rasilimali za kutosha ikiwemo bahari na tuna vijana wenye nguvu ya kufanya kazi katika maeneo yao bado nguvu ya kukimbia ni ndogo ukilinganisha na maeneo mengine”Alisema

Alisema hivyo wanaweza kutumia njia ya mdahalo kujadiliana changamoto ambazo zinaweza kuwasaidia ili jamii ikaendelea na wilaya hiyo kuongeza kipato chake cha mapato kupitia wavuvi na wakulima wa mwani pamoja na sekta nyengine ili kuweza kuimarika kwa kiuchumi.

“Kwa maana kupata mapato ya kutosha kwani sisi kama idara ya maendeleo ya jamii kukiwa na amani tafsiri yake watu watafanya kazi na serikali kupata mapato na hatimaye kurudisha kwa jamii ...amani ilipo ndani ya Halmashauri yetu imepelekea watu kupendana, kuchukuliana kwa madhaifu machache yaliyopo na kukaa pamoja kujadiliana njia madhubuti za kutatua hizo changamoto”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba Migogoro ndio chanzo kikubwa cha kutokuendelea, kwenye amani ndio kwenye maendeleo hata ndani ya nyumba vile mtu alivyo ndani mwake ndio kama wanaweza kutatua changamoto ndani.

Mkuu huyo wa Idara ya Maendeleo ya Jamii alisema wanatambua serikali moja ya jukumu lake kufikisha huduma mbalimbali kwa wananchi kadri inavyowezaekana wakiwemo washirika wa maendeleo wanapotoa mwanya wa kuunga mkono katika kuhakikisha inawafikia wananchi katika maeneo yao.

“Niwashukuru Shirika la Uwashemu kwa kuwa tayari kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha wanatakeleza majukumu yao bila kuvunja taratibu na mmekuwa mkifanya kazi nzuri kwa jamii na inaleta matokea chanya “Alisema

Aliongeza kwamba kupitia mafunzo hayo yenye lengo kutumia dhana ya mdahalo kuhakikisha wanajadiliana kwa pamoja ili kuweza kutatua migigoro inayoweza kujitokeza kwenye jamii kwa ukanda huo wana wavuvi na wakulima wa mwani ni wakati sahihi kuweza kuwasilisha changamoto zilizowakabili pande zote hizo mbili ili kuweza kutoka na suluhisho la kudumu.

“Kwa mana kutatua changamoto zilizopo kwenye meneo yetu ili mkulima wa mwani aweza kuongeza uzalishji wake bila kumuathiri mvuvi ndivyo hivyo kwa wavuvi dhidi ya wakulima bila kugombana”Alisema


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »