Na Amina Omari,Tanga
Kiwanda cha kutengeneza mikate cha (TANGA MODERN BAKERY
)kimekua cha pili kufungiwa shirika la viwango Tanzania TBS katika
kipindi kisichozidi wiki moja mkoani Tanga baada ya kubainika kuwa
kinazalisha mikate bila kufuata taratibu za viwango bora vya uzalishaji.
Akizungumza katika oparesheni hiyo, Afisa Uhusiano wa TBS Rhoida Andusamile
alisema wamezuia uzalishaji katika kiwanda hicho baada ya kubaini kuwa
wamiliki wakiwanda hicho wamekua wakitengeneza mikate ambayo
inatengenezwa bila kufuata taratibu za shirika la viwango nchini.
Alisema mikate ni bidhaa ambayo ipo katika viwango vya lazima vya ubora hivyo kiwanda hicho kwa muda mrefu kimekuwa kinazalisha bidhaa bila kuwa na nembo ya ubora ya kutoka TBS.
“Niwajibu wetu kuhakikisha kila mzalishaji nchini
anazalisha bidhaa zenye ubora kwa lengo la kuwakinga walaji na madhara
ya kiafya hivyo tumekuwa tukiendesha ukaguzi wa mara kwa mara katika
bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini lengo ikiwa ni kumlinda
mlaji”Andusamile.
Nae mkaguzi washirika hilo Deusdedit Paschal alisema bakery hiyo ilitakiwa kabla haijaanza uzalishaji wapeleke sampuli za mikate TBS kwa ajili ya kuangalia ubora pamoja na ukaguzi kufanyika lakini yote hayo hayakufanyika.
Alisema
kwa miaka 16 kiwango hicho kimekuwa kizalisha mikate hiyo pamoja na
bidhaa nyingine kama keki bila ya ya kuwa na mikataba na TBS wala nembo
ya ubora pamoja na ukaguzi.
Kwa upande wake Meneja
wa kiwanda hicho Hilal Salim alikiri kuendesha uzalishaji bila kuwa na
nembo ya kuthibitisha ubora wa bidhaa yake ,hata hivyo alliomba TBS
kutokifungia kiwanda hicho kwani wananchi wengi wataathirika na ukosefu
wa bidhaa zake
Hata
hivyo baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho walisema kufungiwa kwa
kiwanda hicho kutawathiri kiuchumi kwani walikuwa wanatagemea ajira hiyo
kuendesha familia zao.
Mei
22 mwaka huu shirika la viwango nchini TBS lilifungia kiwanda cha
kutengeneza maji cha Al Hayaa kutoka na kuendeleza uzalishaji wa bidhaa
hiyo bila kuwa na leseni ya ubora.
|
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon