Na Boniface Wambura,Dar es Salaam.
Raundi
ya pili ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inaendelea leo (Mei 26 mwaka huu)
kwa mechi sita za kwanza zitakazochezwa katika miji sita tofauti.
Abajalo
ya Dar es Salaam na Kariakoo ya Lindi zitaumana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume, Dar es Salaam wakati Machava FC ya Kilimanjaro itakuwa mwenyeji wa
Mpwapwa Stars ya Dodoma kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.
Nayo
Stand United FC ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Magic Pressure ya Singida kwenye
Uwanja wa Namfua mjini Singida huku Polisi Jamii ya Bunda mkoani Mara ikimenyana
na Biharamulo FC ya Kagera kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.
Mjini
Kigoma kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika ni kati ya wenyeji Saigon FC na Katavi
Warriors ya Katavi wakati Njombe Mji itaikaribisha Kimondo SC ya Mbeya kwenye Uwanja
wa Sabasaba mjini Njombe.
Timu
zitakazofuzu kucheza raundi ya tatu zitacheza mechi za kwanza kati ya Juni 8 na
9 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitakuwa kati ya Juni 15 na 16 mwaka huu.
Mwisho.
EmoticonEmoticon